Home AJIRA Faida za kuwa Freelancer

Faida za kuwa Freelancer

0 comment 174 views

Imekuwa ni kawaida kusikia watu wanataka kujiajiri, au kufanya ujasiriamali kutokana na sababu mbalimbali kwamfano malipo kidogo, ukosefu wa muda wa kufanya shughuli nyingine nk. Kutokana na hayo Intaneti imekuwa ni msaada mkubwa kwa watu katika masuala mbalimbali ikiwa ni pamoja na suala la kuajiri na kuajiriwa. Siku hizi si lazima watu waajiriwe kazi za muda mrefu (Fulltime), hapa ndio suala la ‘Freelance’ linapokuja.

Freelancer ni mtu aliyejiajiri, mara nyingi mtu huyo hutoa huduma kwa wateja mbalimbali na kufanya kazi mbalimbali kwa wakati  mmoja kutokana na utaalamu au ujuzi alio nao. Kikawaida mtu huyo hulipwa kila baada ya kumaliza kazi husika na kazi hizo huwa ni za muda mfupi.

Freelancers wameleta ahueni kwa wafanyabiashara au wamiliki wa kampuni pia hususani katika upande wa utoaji wa ajira. Kwani ikiwa kampuni itaajiri freelancer kampuni hiyo itafanya malipo mara moja tu baada ya kazi kukamilika, jambo ambalo husaidia kuokoa fedha kwani katika upande wa utoaji wa ajira za muda mrefu kampuni hutakiwa kusaini mikataba ya muda mrefu na wafanyakazi na kutakiwa kuwapa malipo ya ziada kwamfano bima ya afya, mishahara wakati wa likizo nk hii inaweza kugharimu fedha nyingi na wakati mwingine kutopata matokeo yaliyokuwa yakitegemewa licha ya kutoa mishahara mikubwa kwa wafanyakazi na faida mbalimbali.

Hivyo basi, zifuatazo ni faida za kuwa freelancer:

Udhibiti katika kazi na wateja

Kikawaida mtu akiwa anafanya kazi katika kampuni fulani huwa si rahisi kuchagua kazi au wateja wa kufanya nao kazi hii inaweza kuwa ni changamoto kubwa ikiwa mtu huyo atapangiwa kufanya kazi na watu wasio wataalamu au wenye kauli mbaya. Lakini kwa kuwa freelancer unakuwa na maamuzi ya kazi unazotaka kuzifanya na aina ya wateja unaotaka kujihusisha nao kutokana na ujuzi au utaalamu ulio nao. Hii husaidia katika ufanisi mzuri wa kazi na kuleta faida kwa mtu aliyekuajiri huku ukitengeneza historia nzuri.

Muda

Katika upande wa muda, kila mtu huwa na muda wake ambao huwa makini zaidi na kuna muda akili hupunguza umakini wa kuzingatia mambo muhimu kwamfano kuna watu wengine huwa makini zaidi alfajiri, na wengine mchana, huku wengine huwa makini zaidi usiku. Hivyo basi, Freelancer ana uhuru wa kufanya kazi zake muda wowote ili mradi kazi hizo zitamfikia mteja katika muda wa makubaliano au kabla ya muda wa makubaliano zikiwa na ubora stahiki.

Eneo la kazi

Inaelezwa kuwa kukaa sehemu moja hupunguza ufanisi wa kazi ndio maana huwa inashauriwa kutenga dakika chache za mapumziko ili kuweza kurudisha umakini. Katika upande wa freelancing, mtu anaefanya kazi hii huamua wapi anataka kufanya kazi zake ili kuweza kufanya kwa ustadi zaidi na kuzimaliza ndani ya muda. Kwamfano mtu anaweza kuchukua likizo huku akiendelea kufanya kazi zake. Kwakifupi katika kazi hii si lazima kukaa sehemu moja ili kuweza kumaliza kazi husika. Jambo la umuhimu ni umakini na ubora pale kazi itakapotimia.

Faida

Haijalishi mradi unaoufanya ni mkubwa au mdogo, ikiwa utakuwa freelancer kazi zote utakazozifanya mapato/faida zote zitakazopatikana hupitia kwako moja kwa moja, bila kupitia kwa watu wengine . Hii  huleta uhuru wa kutumia fedha hizo kujiboresha na kupanua biashara yako.

Baadhi ya kazi ambazo watu wanaweza kufanya kwa muda mfupi(freelance) ni pamoja na upigaji picha, graphic designing, masuala ya kufanya mahesabu (accounting) , utafutaji wa masoko, uhariri wa picha na video, uandishi na kutafsiri nk.

Aidha, ikiwa mtu  anataka kujikita katika tasnia hii ni muhimu kuwa na mipango madhubuti ikiwa ni pamoja na masuala ya utafutaji wa wateja na miradi, kupanga muda wa kazi na muda wa masuala mengine, na kuwa tayari kwaajili ya changamoto mbalimbali ambazo zinaweza kujitokeza.

Inashauriwa kufanya kazi kitaalamu ili kuwahamasisha watu makini kukupa kazi zinazolipa zaidi. Kwamfano ikiwa umehudhuria hafla za kujenga mitandao hakikisha una kadi ya mawasiliano, ili kuweza kuwajulisha watu wa tasnia mbalimbali uwepo wa huduma unayoitoa.

Usisubiri muda muafaka kufanya mambo ambayo unafurahia kuyafanya na unaamini kwa kuyafanya mambo hayo utapata ujuzi zaidi, utakuza mtandao wa biashara yako, utatimiza malengo yako na kufanikiwa. Ajira-(https://ajiras.com/ ) ni  moja ya tovuti iliyopo nchini inayotoa huduma ya kujisajili-kujitangaza kuhusu kazi mbalimbali za Freelance, na hata kampuni mbalimbali zinaweza kupata wafanyakazi wa muda kupitia tovuti hiyo.

 

 

 

 

 

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter