Home BIASHARA Tanzania na ubalozi wa uholanzi wasaini mkataba wa kuboresha na kuendeleza ujasiriamali

Tanzania na ubalozi wa uholanzi wasaini mkataba wa kuboresha na kuendeleza ujasiriamali

0 comment 140 views

Dar es Salaam. Tanzania Startup Association (TSA) na ubalozi wa ufalme wa Uholanzi wametia saini mkataba wa makubaliano kuboresha na kuendeleza sekta ya ujasiriamali nchini.

Mkataba huo una lengo la kuanzisha na kuendeleza mazingira wezeshi ya kisheria na kisera ya kibiashara nchini.

Akizungumza wakati wa utiaji saini jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi mtendaji wa TSA Zahoro Muhaji amesema “tunayo furaha kushirikiana na ubalozi ambao umetambua kazi ya TSA katika kuwakilisha, kutambulisha na kukuza mazingira wezeshi ya kibiashara kwa sekta ya biashara ndogo ndogo na za kati zinazochipukia na kukua kwa kasi.

Amesema sekta hii inayo nafasi ya kubadili maisha na vipato kwa vijana na watanzania kwa ujumla.

Ametaja fursa ya ukuaji na uwekezaji kuwa kikwazo kwa biashara ndogo na za kati zinazochipukia kutokana na ugumu wa upatikanaji wa mikopo, ukosefu wa ujuzi wa matakwa ya kisheria, ujuzi wa kusimamia na kuendesha biashara na undelezaji wa biashara hizo.

Amesema hali hiyo imepelekea udumavu na maendeleo hafifu hivo kuwazuia wawekezaji kuwekeza katika seka hiyo.

“Zaidi udumavu huu umechangiwa na kukosekana kwa sheria mahususi na sera zinazoongoza aina hii ya biashara na nafasi jumuishi ya wadau wa sekta hii,” amesema Muhaji.

Muhaji amebanisha kuwa kumekuwa na ukuaji wa mwamko barani Afrika katika kutumia na kuandaa sera na sheria mahususi zinazotambua na kusimamia biashara ndogo na za kati.

Amezitaja Tunisia na Senegali kuwa nchi mbili za kwanza barani Afrika kuandaa sera na sheria zinazohusu biashara za aina hiyo.

Nchi nyingine kama Mali, Ghana, Kenya, Ivory Coast, jamhuri ya demokrasia ya Kongo na Rwanda zinatarajia kuanza kutumia sera na sheria zao mwaka huu.

Tunapenda kutumia fursa hii ya kisekta katika kuongeza ajira nchini. Hivi karibuni kumekuwa mwamko wa biashara za aina hii katika kutatua tatizo la ajira hapa nchini.

Balozi wa Uholanzi nchini Tanzania Jeroen Verheul amesema, “lengo letu sio tu kuendeleza sekta ya nyumbani bali kwingineko duniani. Kuwezesha mazingira rafiki ya kibiashara, kisheria na kisera hususani Tanzania,”.

Balozi Verheul amesema sheria bora zinachagiza maendeleo na kuondoa vikwazo ambavyo vinadumaza maendeleo ya kibiashara.

Sheria hizi zitaongeza kujiamini, kukuza nguvu kazi, kudumisha ubunifu na maendeleo endelevu, ikivutia uwekezaji, upatikanaji fedha na elimu.

Sheria ya usimamizi wa biashara ndogo na za kati zinazochipukia ambazo zitaundwa kwa kushirikia na TSA, wadau mbalimbali pamoja na ubalozi zitakuwa nyenzo muhimu ya kutambua na kujibu changamoto katika maswala ya maendeleo ingawa utafiti katika nchi nyingine za Afrika umeonyesha swala hili linahitaji muda mrefu na ushirikishwaji mkubwa wa wadau mbalimbali.

Tunaamini TSA kama mdau katika sekta hii Tanzania tuna nafasi ya kuleta mabadiliko tukishirikiana na wadau wengine katika mchakato huu.

Serikali ya Uholanzi imetambulika duniani kote kama kiongozi wa kisekta na biashara wenye zaidi ya makampuni 4000 ikishika nafasi ya tano duniani kwa kiwango cha ubunifu kwa mujibu ya ripoti ya Global Innovation Index.

Makampuni hayo yamefaidika na kunufaika na mazingira rafiki ya kisera na kibiashara yenye ubora uliothibitika duniani.

TSA ilianzishwa rasmi mwezi mmoja uliopita na umekuwa mwavuli wa ushirika wa wanachama wa wamiliki wa biashara ndogo na za kati zinazokuwa kwa kasi, wenye lengo la kuwaleta pamoja wadau wa sekta hii nchini.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter