Home BENKI Benki ya Afrika yampongeza Magufuli uimara wa uchumi Tanzania

Benki ya Afrika yampongeza Magufuli uimara wa uchumi Tanzania

0 comment 118 views

Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) imempongeza Rais John Magufuli kwa uthubutu ulioiwezesha Tanzania kuwa miongoni mwa nchi yenye uchumi unaokuwa kwa kasi barani Afrika licha ya janga la virusi vya corona.

Rais wa AfDB Dk. Akinwumi Adesina amesema “kwanza napenda kumpongeza rais Magufuli kwa kuchaguliwa tena. Rais Magufuli ni mtendaji. Sasa hivi ukizungumzia suala la miradi haipungui kwake, ni mtu mwenye kasi, humaliza miradi na kufanya mingine”.

Rais Adenisa, alitoa pongezi hizo wakati wa salamu fupi kuhusu uimara wa uchumi wa tanzania na pongezi kwa rais Magufuli.

Kuhusu ukuaji wa uchumi wa Tanzania alisema nchi ilifanikiwa katika ukuaji wa Pato la Taifa (DGP) la asilimia 6.9 mwaka 2019.

Alisema “wakati ukuaji wa uchumi uliposhuka barani Afrika hadi asilimia -2.1 mwaka 2020 kutokana janga la Corona, Tanzania bado imeweza kurekodi ukuaji wa asilimia 2.1, hilo ni jambo kubwa sana. Benki ya Maendeleo Afrika ilitabiri kuimatika kwa uchumi Tanzania mwaka 2021”.

Ukuaji halisi wa Pato la Taifa unatarajiwa kuongezeka hadi asilimia 4.1 mwaka 2021 na utaongezeka mpaka asilimia 5.8 mwaka 2022. Aliongeza kuwa Tanzania ni nchi inayostahimili na yenye misingi madhubuti ya uchumi.

Aidha, aliwataka viongozi wengine barani Afrika watambue kuwa rais Magufuli ni mtu wa kucdhukua hatua hassa linapokuja swala la utekelezaji wa miradi ya maaendeleo kwa wananchi.

 

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter