Home AJIRA Ni aibu kijana kukaa bila kazi : Rais Samia

Ni aibu kijana kukaa bila kazi : Rais Samia

0 comment 117 views

Rais Samia Suluhu amesema Tanzania ina fursa nyingi za ajira lakini vijana wengi wanasubiri kuajiriwa wanapomaliza masomo.

Rais Samia amesema hayo Januari 07, 2022 katika maadhimisho ya Kilele cha Matembezi ya Miaka 58 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.

“Vijana wengi tukimaliza kusoma tunasubiri ajira, lakini hatuhangaiki kutafuta fursa za kazi, kazi ziko nyingi sana Tanzania, ni vijana kuchakarika kuziona hizo fursa na kuanza kuzitumia,” amesema Rais Samia.

“Tunaelewa kwamba vijana wetu hawa wanakabiliwa pia na tatizo la ukosefu wa ufundi stadi na stadi za kazi, kwamba kijana anamaliza shule yake lakini anakaa na vyeti vyake kusubiri ajira ya serikali. Na hii ni kwa sababu hatujawatayarisha vya kutosha kujua stadi za kazi na kupata ule utaalamu,” ameeleza Rais.

“Lakini nataka niwaambie kwamba ndani ya miezi 9 ya awamu ya sita, takwimu za ajira kwa ujumla wake zinapaa kufika 14,000.

Amebainisha kuwa serikali inajua tatizo la ajira na inajitahidi kutengeza fursa mbalimbali ili vijana wapate ajira.

Kuhusu changamoto ya Mitaji amesema ipo Mifuko inayotoa Mikopo kwa vijana, lakini bado haijatosheleza kutokana na idadi yao kuwa kubwa

Amesema vijana ni nguzo muhimu sana katika kuleta maendeleo ya taifa lolote duniani.

Kwa mujibu wa sensa ya mwaka 2012, katika kila idadi ya watu 10 Tanzania kati yao wanne ni vijana wenye umri kati ya miaka 15 hadi 35 hivyo inafanya Tanzania kukadiriwa kuwa na vijana milioni 21.

Soma zaidi:

Wahitimu vyuo vikuu wanavyoomba kazi za elimu ya sekondari

Mitandao ya kijamii na fursa kiuchumi

Vikundi vya wajasiriamali vyakabidhiwa hundi ya bilioni 2

Kuna uwezekano nusu ya ajira kutoweka 2050

 

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter