Home Elimu Rais Samia azindua taasisi Zanzibar

Rais Samia azindua taasisi Zanzibar

0 comment 173 views

Takwimu zinaonyesha ufaulu hafifu kwa watoto wa kike visiwani Zanzibar.

Hali hiyo inakwamisha maendeleo ya haraka kwa mtoto wa kike na jamii nzima kwa ujumla.

Taasisi ya Mwanamke Initiative (MIF) imetazama tatizo la changamoto ya ufaulu kwa watoto wa kike katika visiwa hivyo na kuja na suluhu ya kutaka kumaliza tatizo hilo.

Juni 19, Rais Samia Suluhu Hassan amezindua taasisi hiyo visiwani Zanzibar katika hoteli ya Golden Tulip.

Uzinduzi huo ulihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa kitaifa kutoka Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.

Rais Samia amesema “jambo linalofanya na wenzetu wa MIF ni jambo la kizalendo, linalopaswa kuungwa mkono na wadau mbalimbali kwani sote tunafahamu kuwa ukimwezesha mwanamke umeiwezesha jamii nzima hivyo taasisi hii inakwenda kuikomboa jamii nzima kupitia juhudi ambazo inafanya kwa mtoto wa kike.”

Ameeleza kuwa kufunguliwa kwa taasisi hiyo ni jambo moja lakini kutatua changamoto zilizopo ni jambo lingine, hivyo ameipongeza MIF kwa kuonyesha nia ya dhati.

Fatma Mwassa ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa MIF amesema taasisi itajihusisha na ukombozi wa mwanamke kupitia uwezeshaji wa kielimu, afya na sekta ya kilimo.

“MIF kupitia mpango mkakati wake wa miaka mitano inakusudia kuwa na kituo kitakachoshughulika na watu wenye changamoto za afya ya akili na ulemavu wa kiakili, eneo ambalo mara nyingi husahaulika na nguvu nyingi kuwekezwakwa watu wenye ulemavu wa viungo tu,” ameeleza Fatma.

Pamoja na kuzinduliwa kwake, taasisi ya MIF tayari imefanikiwa kutekeleza miradi kadhaa ikiwemo kutoa ufadhili wa masomo kwa wanafunzi bora wawili wasichana ambao watasomeshwa mpaka pale watakapofika kikomo cha elimu yao.

“Sambamba na hilo MIF imetoa ufadhili wa masomo kwa wanafunzi 10 walioshika nafasi 10 za juu kupata masomo nje ya nchi (Scholarship) kwa wasichana.

“Mpaka sasa MIF imefanikiwa kuwapeleka wanafunzi zaidi ya 100 katika vyuo vya ufundi Tanzania Bara. Inakusudia kujenga vyoo 150 katika shule mbalimbali nchini ambavyo kati ya hivyo 75 vitajengwa Tanzania Bara.”

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter