Home VIWANDA Mifuko ya Jamii kuimarisha uchumi wa viwanda

Mifuko ya Jamii kuimarisha uchumi wa viwanda

0 comment 113 views
Na Mwandishi wetu

Katibu wa Umoja wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii Tanzania (TSSA) Meshack Bandawe amesema kuwa umoja huo unakusudia kufufua viwanda 25 vilivyoshindwa kujiendeleza kwa takribani miaka 20 kama njia mojawapo ya kuitikia wito wa serikali wa kuifanya Tanzania kuwa nchi ya viwanda.

Bandawe ambaye pia ni Meneja wa Mfuko wa Pensheni wa PPF katika mikoa ya kanda ya ziwa amesema hatua hiyo inalenga kukuza uchumi wa nchi, kuibua ajira zaidi katika sekta ya viwanda hapa nchini na pia kuboresha viwango vya bidhaa zinazozalishwa ili kukabiliana na ushindani katika soko la ndani na hata la Afrika Mashariki.

Ametaja baadhi ya mifuko inayoshiriki katika mchakato huo kuwa ni Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF), Mfuko wa Pensheni wa Watumishi wa Serikali za Mitaa (LAPF), Mfuko wa Pensheni wa Watumishi wa Serikali Kuu (GEPF), Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma (PSPF) pamoja na Shirika la Hifadhi ya Jamii Zanzibar (ZSSF).

Mbali na kufufua viwanda vilivyoshindwa kujiendeleza, Bandawe ameongeza kuwa mifuko hiyo pia inatarajiwa kuanzisha viwanda vipya maeneo mbalimbali kote nchini ili kuchochea kasi ya ukuaji wa uchumi.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter