Home VIWANDA Tsh bilioni 3.4 kujenga kiwanda cha kubangua korosho

Tsh bilioni 3.4 kujenga kiwanda cha kubangua korosho

0 comment 71 views

Shilingi bilioni 3.4 zinatumika kujenga kiwanda cha kugangua korosho Newala mkoani Mtwara.

Ujenzi wa kiwanda hicho ni matokeo ya kuwa na ushirika imara wa Chama Kikuu cha Ushirikia cha TANECU Ltd.

Kiwanda hicho kimezinduliwa rasmi na Waziri wa Kilimo Hussein Bashe Oktoba 1, 2024 ambapo maelfu ya wakulima wameshuhudia kwa hamasa za uhakika wa soko la mavuno ya korosho zao.

Waziri Bashe ambaye yupo mkoani Mtwara kwa ziara ya kikazi amekipongeza Chama Kikuu cha Ushirika cha TANECU Ltd. kwa kuwa mfano mzuri wa kuonesha ushirika unaozidi kuwa imara kwa kuhakikisha uwekezaji huo wa kiwanda ni wa wakulima wenyewe.

“Naelekeza pia kijengwe kiwanda kingine kama hiki kule Tandahimba ili kiwe tayari wakati wa msimu wa mwaka ujao,” amesema Waziri Bashe.

Kiwanda cha TANECU kina uwezo wa kubangua tani 3,500 kwa mwaka.

Mkakati ni kuwa na viwanda 20 vya Kubangua Korosho chini ya TANECU katika mkoa wa Mtwara ambapo 10 vitajengwa Newala (tayari 1 kimezinduliwa) na 10 vitajengwa Tandahimba.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter