Home BENKI BoT kuja na mfumo mpya utekelezaji sera ya fedha

BoT kuja na mfumo mpya utekelezaji sera ya fedha

0 comment 120 views

Benki Kuu ya Tanzania (BoT) inatarajia kubadilisha mfumo wa sasa wa utekelezaji wa sera ya fedha ambao unatumia ujazi wa fedha na kuanza kutumia mfumo mpya unaotumia riba ya Benki Kuu (Central Bank Policy Rate).

Taarifa ya Benki Kuu inasema mfumo huo unatarajiwa kuanza mwezi Januari 204.

“Hii ni katika jitihada za kuboresha ufanisi wa utekelezaji wa sera ya fedha na kusimamia malengo mapana ya kiuchumi ya kudumisha utulivu wa bei na ukuaji wa uchumi,” imesema taarifa ya Gavana wa BoT.

Taarifa hiyo inaeleza kuwa, utekelezaji wa Mfumo wa Riba ya Benki Kuu umeonesha matokeo mazuri katika usimamizi wa sera ya fedha na kuimarisha misingi ya utekelezaji wake katika mazingira ya uwazi katika nchi zinazotumia mfumo huo.

Mfumo huo ambao ulianza kutumika duniani mwaka 1990, hadi sasa unatumiwa na Benki Kuu za nchi 45.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter