Home BIASHARA Dondoo tano zitakazo kusaidia kukuza biashara ndogo

Dondoo tano zitakazo kusaidia kukuza biashara ndogo

0 comment 53 views

Ili kufanikiwa katika jambo lolote, kuna mambo kadhaa wa kadhaa ya kuzingatia. haya ni mambo matano ambayo yanaweza kukusaidia kukuza biashara yako.

Wajue wateja wako

Boresha bidhaa na huduma zako. Hii itasaidia kuwavutia wateja wako na kupata mafanikio. Pia kufanya utafiti kujua ni nini mteja anahitaji ni njia rahisi ya kupata wateja wengi na kwa muda mfupi.

Boresha huduma kwa wateja

Huduma bora kwa wateja ni nguzo muhimu ya kuzingatia katika biashara. Kukosekana kwa huduma bora kunaweza kusababisha kutowaridhisha wateja wako hata kama una bidhaa nzuri. Wateja wanapenda kuhudumiwa vizuri, na katika biashara hii huwafanya wateja wajisikie wa kipekee.

 Jenga uaminifu

Kama ndio unaanza biashara itachukua muda kiasi kuwashawishi wateja kununua bidhaa zako. Lakini kuwafanya wanunue pekee haitoshi.

Unatakiwa kuwa na uaminifu ukijua kuwa kuna wapinzani katika hiyo biashara ambao wanaweza kutoa bidhaa bora zaidi. Inakubidi kuwa makini zaidi ili wapinzani wasikuzidi na kuchukua wateja wako kiurahisi. Mathalani kama katika biasahara yako pia unatoa huduma ya kutuma bidhaa sehemu mbalimbali (delivery) hakikisha unaifanya kwa uaminifu mkubwa. Mteja anapochagua bidhaa, hakikisha unamtumia ile ile alioichagua na kwa uaminifu mkubwa. Baadhi ya wafanya biashara huwa wanashindwa kuwa waaminifu katika hili. Wengine hawatumi mzigo kwa wakati huku wengine wanapokea malipo kutoka kwa wateja na hawawatumii wateja bidhaa zao, kwa lugha jingine hii tunaita utapeli, hili ni jambo la kuliepuka kabisa kwani litakupotezea wateja na kukuharibia jina lako.

Matumizi ya mitandao ya kijamii

Kwa sasa dunia imekuwa ya kijidigitali. Matumizi ya mitandao ya kijamii ni nguzo muhimu katika biashara. Ukitumia mitandao ya kijamii ikiwemo Facebook, twitter, instagram, WhatsApp na mingineyo kutangaza biashara yako itakusaidia kufikia watu wengi kwa wakati mmoja.

Hakikisha unatumia mitandao ya kijamii vizuri kwa kutangaza na kuonesha bidhaa yako. Kupitia mitandao hiyo, utaweza kupata maoni ya watu nah ii itakufanya ujue wanataka nini hasa na sok linataka nini na wapi pa kuboresha katika biashara yako. Hii pia itakufanya kuwajua vema wateja na kuwapa kile wanachokitaka.

Hudhuria warsha na kujenga mtandao wa biashara

Ukipata nafasi ya kuhudhuria warsha, semina au mikutano mbalimbali inayohusu masuala ya biashara usiipoteze. Hii ni fursa ya kukuza mtandao wako wa biashara na kujenga mahusiano. Unapokutana na wafanyabiashara wengine iyakusaidia kujifunza mambo tofauti na kupata ujuzi mpya wa kukuza na kuboresha biashara yako kwa viwango vya juu.

Wajasiriamali wengi huwa hawatumii fursa hii ipasavyo. Kw kuhudhuria mikutano na warsha mbalimbali itakusaidia kukutana na wateja wapya, wafanyakazi na hata wawekezaji.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter