19
Nchi zilizoendelea zimetakiwa kutimiza ahadi yao ya kutoa dola za marekani bilioni 500, sawa na dola bilioni 100 kila mwaka kwa ajili ya kuzisaidia nchi zinazoendelea kukabiliana na changamoto za mabadiliko ya tabianchi katika kipindi cha miaka mitano, kuanzia mwaka 2020 hadi mwaka 2025.
Waziri wa Fedha Dkt. Mwigulu Nchemba amesema hayo wakati akichangia hoja katika Mkutano wa Ngazi ya Juu wa Mawaziri uliojadili namna ya kupata fedha kwa ajili ya kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi, pembezoni mwa Mkutano wa 29 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Nchi Wanachama wa Mkataba wa Umoja wa Mataifa kuhusu Mabadiliko ya Tabianchi (COP-29) unaofanyika katika Mji wa Baku, nchini Azerbaijan