Naibu Waziri wa Kilimo Dk. Mary Mwanjelwa amesema serikali imejipanga kutoa miche ya mikorosho bure kwa wakulima wa mikoa ya Pwani, Lindi na Mtwara baada ya ugonjwa wa Mnyauko Fusari kusambaa kwa kasi na kuathiri takribani mikorosho 71,512 katika wilaya ya Mkuranga. Dk. Mwanjelwa amesema jitihada za haraka zinahitajika ili kunusuru zao la korosho na serikali imejipanga kulifanyia kazi tatizo hilo kwani kilimo cha korosho kimekuwa chanzo kizuri cha serikali kujipatia fedha za kigeni na wakulima kukuza uchumi.
Akizungumzia suala hilo, Fortunatus Kapinga ambaye ni Kaimu mtafiti wa korosho wa kituo cha Naliendele amesema kuwa tayari miche ambayo itatolewa bure imeshafanyiwa utafiti na wataalamu wanaendelea kutafuta ufumbuzi wa ugonjwa huo ambao tatizo lake linasemekana kuwa kwenye udongo