Home BIASHARAUWEKEZAJI Dodoma yafungua fursa za uwekezaji

Dodoma yafungua fursa za uwekezaji

0 comment 223 views

Serikali ya Tanzania imekuwa na mpango wa kuhamisha makao makuu ya nchi kwenda Dodoma kwa takribani miaka 40 sasa. Hata hivyo, serikali ya awamu ya tano imeonyesha dhamira ya dhati ya kutekeleza mpango huo ambapo hadi sasa, asilimia 70 ya ofisi za serikali tayari zimekisha fanya hivyo. Ni wazi kuwa mabadiliko haya yatagharimu fedha nyingi mpaka kukamilika kwake lakini pia yatakuwa na faida nyingi hususani kwa wakazi wa jiji la Dodoma. Hizi hapa ni baadhi ya faida za serikali kuhamia Dodoma na kutangaza rasmi kuwa mji huo sasa utakuwa jiji.

Msongamano utapungua kwa kiasi kikubwa jijini Dar es salaam. Kutokana na jiji hili kuwa makao makuu ya serikali kwa kipindi kirefu sana, watu kutoka mikoa mbalimbali wamekuwa wakisafiri kufuata huduma za kiserikali, jambo ambalo limekuwa likisababisha msongamano wa watu katika maeneo mengi huku kukiwa na changamoto kubwa ya foleni. Huduma hizi zikisogezwa karibu zaidi, msongamano utapungua jijini Dar es salaam kwa kiasi kikubwa hivyo watu watapata muda mwingi zaidi kufanya shughuli za kimaendeleo.

Miundombinu itaboreshwa kwa kiasi kikubwa Dodoma. Serikali imejipanga kujenga reli ya kisasa itakayotoa huduma ya usafiri wa mwendo kasi kutoka Dar es salaam hadi Dodoma, kujenga uwanja wa ndege na vilevile kuboresha barabara ili kurahisisha usafiri. Hii yote itakuwa neema kubwa kwa wakazi wa Dodoma na maeneo jirani kwani shughuli zao za kibiashara zitafanyika kirahisi zaidi.

Mbali na hayo, kitendo cha serikali kuhamia Dodoma kutaongeza mzunguko wa fedha katika mji huo kwa kiasi kikubwa hivyo kutakuwa na fursa zaidi za ajira pamoja na uwekezaji. Vijana wengi zaidi watapata nafasi ya kujiendeleza kiuchumi kwani safari ya serikali Dodoma italeta fursa mbalimbali kwao hivyo kuwatoa katika hatua waliopo sasa na kwenda katika bora zaidi kimaisha.

Mabadiliko haya yanakuja na fursa mbalimbali ambazo zitawainua wananchi kiuchumi hivyo ni wakati muafaka wa wananchi kutumia hii nafasi kwa ajili ya kujiendeleza kiuchumi. Hivyo uamuzi wa serikali kuhamia Dodoma unabeba faida nyingi kwa wakazi wa jiji hilo kimaendeleo. Ni muda mzuri kwa wawekezaji kuwekeza zaidi Dodoma, wafanyabiashara kuboresha biashara pamoja na huduma zao na vilevile wajasiriamali kujitangaza zaidi ili wajulikane na taasisi mbalimbali za kiserikali.

 

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter