Home BIASHARAUWEKEZAJI Obama aahidi kuitangaza Tanzania

Obama aahidi kuitangaza Tanzania

0 comment 112 views

Rais Mstaafu wa Marekani Barack Obama ameeleza kuridhishwa na vivutio vya utalii katika hifadhi ya taifa ya Serengeti. Waziri wa Mambo ya Nje, Augustine Mahiga alisema hayo jana alipozungumza na waandishi wa habari baada ya kuzungumza faragha na Rais Obama kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimatifa wa Kilimanjaro (KIA)

Dk. Mahiga amesema Obama ameahidi kuisaidia Tanzania kuvutia wawekezaji katika hifadhi hiyo ambayo yeye pamoja na familia yake wameitembelea.

“Alikuja kutembelea hifadhi ya Serengeti kwa safari binafsi hivyo ni lazima tuheshimu hilo” Alisema

Balozi Mahiga pia ameeleza kuwa, Rais Magufuli amempa Obama zawadi ya picha maalum ya tukio la nyumbu wahamao katika hifadhi ya taifa ya Serengeti ambalo ni la kipekee duniani. Naye Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Anna Mghwira aliyekuwepo KIA amesema ziara ya Rais Obama na familia yake itatangaza vyema utalii wa hapa nchini.

Kwa upande wake, Meneja Uhusiano wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) Pascal Shelutwete amesema ziara ya Rais huyo wa zamani wa Marekani imetokana na jitihada za uhifadhi na kutangazwa vyema kwa vivutio vilivyopo nchini Tanzania.

Aidha baada ya Rais Obama, imeelezwa kuwa Rais wa Uswisi, Alain Berset na familia yake wapo nchini kutembelea vivutio vya utalii. Waziri Mahiga amesema kiongozi huyo atakuwa nchini kwa siku 10 na kwamba atakuwa Tanzania bara kwa siku tano na kwa siku nyingine tano atakuwa Zanzibar. Kiongozi huyo anatarajia kutembelea hifadhi za taifa za Serengeti na Ngorongoro kabla ya kwenda visiwani Zanzibar.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter