Home VIWANDAMIUNDOMBINU Tabora kunufaika na mradi wa maji

Tabora kunufaika na mradi wa maji

0 comment 38 views

Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Profesa Makame Mbarawa amewaagiza makandarasi wanaojenga mradi wa maji kutoka Ziwa Victoria kuhakikisha wanakamilisha mradi huo ifikapo Novemba mwakani.

 

Akizungumza baada ya kukagua ujenzi na ulaziji wa mabomba katika miji ya Tabora, Nzega na Igunga utakaogharimu kiasi cha Sh. 600 Milioni, Prof. Mbarawa amesema wananchi wanahitaji maji kwa kuwa wameteseka na kuhangaika kwa muda mrefu.

 

Waziri huyo amewataka makandarasi hao kuhakikisha wanakamilisha mradi huo kwa wakati licha ya muda wa mkataba huo kufikia tamati  kuwa Februari mwaka 2020.

 

“Wananchi wa mkoa wa Tabora wana hamu kubwa ya kuona mradi huu ukikamilika hata kesho, lakini tuhakikishe umekamilika Novemba mwakani,” Amesema Profesa Mbarawa.

 

Akizungumzia agizo hilo, Meneja Mradi wa Afcons JV, Dhaval Soni amesisitiza watafanya kila linalowezekana kuhakikisha wanamaliza mradi kama alivyoagiza Waziri Mbarawa.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter