Home KILIMO Wakulima wa mahindi wala hasara

Wakulima wa mahindi wala hasara

0 comment 134 views

Naibu Waziri wa Kilimo Omary Mgumba amesema takribani tani milioni moja na laki tatu za mahindi nchini zimekosa soko baada ya jitihada za serikali kutafuta soko kushindikana na hivyo kupelekea wakulima kupata hasara na kushindwa kurudisha gharama ambazo wamewekeza katika katika kilimo chao.

Mgumba amesema hayo jijini Mbeya katika kilele cha maadhimisho ya siku ya wakulima ya nanenane ambapo baadhi ya wadau wa sekta ya kilimo wametoa wito kwa serikali kuongeza nguvu zaidi katika kutafuta masoko kwani uzalishaji umeongezeka tofauti na miaka ya nyuma kutokana na wakulima kuelimika na kuanza kutumia mbegu pamoja na teknolojia bora za kilimo.

Naye Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Albet Chalamila amesema ubovu wa miundombinu ya barabara vijijini unachangia kwa kiasi kikubwa mazao ya wakulima kukosa soko. Naye Naibu Waziri wa nchi, Ofisi ya Rais Tawala za mikoa na serikali za mitaa Joseph Kandege ametoa wito kwa kwa wakuu wa mikoa kutafuta wawekezaji wa viwanda vya kuongeza thamani mazao ili kuwasaidia wakulima kupata masoko kwa bei nzuri.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter