Mabinti takribani 40 kutoka kata tano za wilaya ya Tarime mkoani Mara wamepatiwa mafunzo kuhusu sifa,mbinu na dhana bora za ujasiriamali kwa lengo la kujikomboa kiuchumi na kupunguza utegemezi.
Mabinti hao ambao hawakubahatika kupata elimu kutokana na changamoto mbalimbali kama mimba,ndoa za utotoni na ukeketaji,wamepatiwa elimu hiyo kwa ushirikiano wa shirika la jukwaa na utu wa mtoto (CDF-TARIME) na shirika la Plan International Tanzania chini ya ufadhili wa shirika la Maendeleo la Sweden (sida) na shirika la Umoja wa Watu wa Ulaya (European union) ambayo itadumu kwa siku tatu ikiambatana na elimu ya kupinga ndoa za utotoni,ukeketaji na ukatili wa kijinsia.
Mbali na kupewa elimu hiyo pia mabinti hao wamekua wakipewa vifaa mbalimbali vya ujasiriamali kulingana na aina ya biashara wanazofanya kama vile cherehani,vyombo na vinginevyo lengo likiwa na kukuza biashara zao..