Home BENKI Standard Chartered yawezesha SGR

Standard Chartered yawezesha SGR

0 comment 102 views

Benki ya Standard Chartered Group imeamua kuipatia serikali ya Tanzania mkopo wenye masharti nafuu wa Dola za Marekani bilioni 1.46 sawa na shilingi trilioni 3.3 kwa ajili ya kuendeleza kipande cha reli ya kiwango cha kimataifa (Standard Gauge) kuanzia Morogoro hadi makutupola mkoani Dodoma.

Waziri wa Fedha na Mipango Dk. Philip Mpango amebainisha hayo baada ya kukutana na kufanya mazungumzo na Bill Winters ambaye ni mkurungenzi mtendaji wa benki hiyo jijini Dar es salaam.

Mbali na kuishukuru benki hiyo kwa kukubali kugharamia ujenzi huo, Dk. Mpango amesema lengo la SGR ni kuimarisha usafirishaji wa abiria na mizigo kwenda nchi jirani hasa za maziwa makuu na zile ambazo hazipakani na bahari.

Pia Dk. Mpango amemweleza kiongozi huyo kuhusu vipaumbele vya serikali ikiwemo ujenzi wa mradi wa kufua umeme wa Mto Rufiji pamoja na uboreshaji wa Shirika la Ndege la Air Tanzania (ATCL) lengo likiwa ni kuongeza idadi ya watalii ambao licha ya Tanzania kuwa ya pili kwa vivutio vya utalii lakini hupokea idadi ndogo ya watalii kwa mwaka hivyo nchi hukosa fedha za kigeni.

Benki ya Standard Chartered ni miongoni mwa benki zenye mafanikio huku ikiwa na matawi takribani katika nchi 60 duniani.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter