• Home
  • FEDHA
    • MIKOPO
    • BIMA
    • HISA
  • BENKI
  • BIASHARA
    • UJASIRIAMALI
    • UWEKEZAJI
    • BIASHARA NDOGO NDOGO
  • VIWANDA
    • MIUNDOMBINU
    • NISHATI
    • UZALISHAJI
  • KILIMO
    • KILIMO BIASHARA
    • KILIMO UFUNDI
  • MAHOJIANO
  • AFRIKA MASHARIKI
    • BIASHARA
    • FEDHA
    • UJASIRIAMALI
Sunday, January 29, 2023
  • Login
  • Home
  • FEDHA
    • MIKOPO
    • BIMA
    • HISA
  • BENKI
  • BIASHARA
    • UJASIRIAMALI
    • UWEKEZAJI
    • BIASHARA NDOGO NDOGO
  • VIWANDA
    • MIUNDOMBINU
    • NISHATI
    • UZALISHAJI
  • KILIMO
    • KILIMO BIASHARA
    • KILIMO UFUNDI
  • MAHOJIANO
  • AFRIKA MASHARIKI
    • BIASHARA
    • FEDHA
    • UJASIRIAMALI
No Result
View All Result
Pesatu
  • Home
  • FEDHA
    • MIKOPO
    • BIMA
    • HISA
  • BENKI
  • BIASHARA
    • UJASIRIAMALI
    • UWEKEZAJI
    • BIASHARA NDOGO NDOGO
  • VIWANDA
    • MIUNDOMBINU
    • NISHATI
    • UZALISHAJI
  • KILIMO
    • KILIMO BIASHARA
    • KILIMO UFUNDI
  • MAHOJIANO
  • AFRIKA MASHARIKI
    • BIASHARA
    • FEDHA
    • UJASIRIAMALI
No Result
View All Result
Pesatu
No Result
View All Result

African Export Import kuipatia Tanzania zaidi ya Shilingi trilioni moja kugharamia ujenzi wa reli na vituo vya biashara

Patricia Richard by Patricia Richard
October 12, 2018
in FEDHA
0
Waziri wa Fedha na Mipango Dk Philip Mpango (Wa kwanza kushoto)

Waziri wa Fedha na Mipango Dk Philip Mpango (Wa kwanza kushoto)

Share on FacebookShare on Twitter

Na: WFM,  Mjini Bali Indonesia

African Export Import Bank (Afreximbank) ya Misri, imeonyesha nia ya kuipatia Tanzania mkopo wa zaidi ya Shilingi trilioni moja (dola za Marekani zaidi ya milioni 500) kwa ajili ya kutekeleza miradi ya kipaumbele hasa ya miundombinu ya reli na kujenga vituo vya biashara (SEZ and Industrial parks).

ADVERTISEMENT

Hayo yalibainishwa mjini Bali Indonesia, na Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Isdor Mpango baada ya Mkutano na Makamu wa Rais wa Afreximbank Bw. Amr Kamel,  uliofanyika  wakati wa mikutano ya mwaka  ya Benki ya Dunia (WB) na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) ikiendelea.

Waziri Mpango, alisema kuwa Afreximbank imethibitisha kuwa ipo tayari kutoa mkopo wa  dola za Marekani milioni 125  (takribani Shilingi bilioni 285.9) kwa ajili ya ujenzi wa reli ya kati kwa kiwango cha Kimataifa  (SGR),  kipande cha Morogoro hadi Makutupora mkoani Dodoma.

“Afreximbank wanania pia ya kutoa  dola milioni 400 (takribani Sh. Bilioni 914.9) ambazo wanaweza kutukopesha kwa ajili ya kugharamia miradi ya miundombinu itakayorahisisha biashara kati ya Tanzania na nchi jirani na Bara la Afrika kwa ujumla,  ili kuchochea kasi ya ukuaji wa biashara katika nchi hizo kwa lengo la kuondoa umasikini”, aliongeza Dkt. Mpango.

Alisema kuwa kwa kuwa tayari Tanzania ilikuwa na mkakati wa kufungua vituo vya biashara katika mikoa ya Dar es Salaam, Mtwara na mikoa mingine, suala la mkopo huo ni fursa kubwa kwa  maendeleo ya nchi, hivyo jambo hilo litafanyiwa kazi kwa kushirikiana na Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji  na Sekta Binafsi, ili Taifa liweze kunufaika na fedha ambazo benki hiyo ipo tayari kuzitoa.

Aidha, amesema kuwa  katika majadiliano na benki hiyo kuna umuhimu wa kuangalia namna ya rasilimali fedha ambazo Benki Kuu za nchi mbalimbali za Afrika zimekuwa zikiwekeza nje ya Bara hilo, ili ziweze kuwekezwa kwenye benki za Afrika kama Afreximbank ili kuleta maendeleo kwa haraka katika Bara hilo.

Vile vile benki hiyo imeikaribisha Tanzania kushiriki mkutano wa biashara utakaofanyika mwezi Desemba mwaka huu mjini Cairo Misri, ambapo kwa upande wa Tanzania ni fursa kwa Makampuni ya umma na binafsi kutangaza bidhaa mbalimbali zinazozalishwa kwa lengo la kukuza biashara ndani ya Bara la Afrika.

Makamu wa Rais wa Afreximbank Bw. Amr Kamel, alisema kuwa Tanzania ni miongoni mwa nchi za kimkakati kwa kuwa ina mchango mkubwa katika maendeleo ya nchi jirani, hivyo Afreximbank imeamua kusaidia miradi mbalimbali ya ujenzi wa miundombinu ili kuharakisha maendeleo ya nchi ya Tanzania na nyingine.

Waziri Dkt. Mpango ameishukuru Benki hiyo kwa kuisaidia Tanzania katika mkakati wa kufikia uchumi wa kati unaotegemea viwanda ifikapo mwaka 2025, hivyo kuwa Taasisi yenye tija si tu kwa maendeleo ya Tanzania lakini pia kwa Bara la Afrika.

Tags: African Export Import BankbiasharaDk. Philip MpangomaendeleomkopoSGRuchumi
Patricia Richard

Patricia Richard

Next Post
Kongamano uwezeshaji kufanyika Juni 15

Fukwe sasa kuchochea utalii

Discussion about this post

Habari Mpya

Poland kuisaidia Tanzania kuweka mifumo ya kodi kidigitali

January 26, 2023

Kamati ya bunge yahimiza uwekezaji maeneo ya hifadhi

January 21, 2023

Serikali kuanzisha mnada wa chai

January 20, 2023

Tumieni bandari ya Dar es Salaam: Makalla

January 19, 2023
Rais Samia Suluhu Hassan akizungumza katika Jukwaa la Uchumi Duniani.

Sekta ya kilimo kukua kwa 10% 2030: Rais Samia

January 19, 2023

Ndege tano kuwasili mwaka huu

January 17, 2023

KUHUSU SISI

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905. PesaTu inamlenga kila mtu ambaye kwa namna moja au nyingine anaguswa na anapenda kujua/ kufuatilia masuala mbalimbali ya kiuchumi ya nchi ikiwemo ujasiriamali, uwekezaji, viwanda, kilimo na hisa.

LATEST

Poland kuisaidia Tanzania kuweka mifumo ya kodi kidigitali

by Pesatu Reporter
January 26, 2023
0

Poland imeahidi kuisadia Tanzania kuimarisha mifumo ya kodi kwa njia ya kidigitali ili kuongeza ufanisi katika ukusanyaji wa mapato ya...

Kamati ya bunge yahimiza uwekezaji maeneo ya hifadhi

by Pesatu Reporter
January 21, 2023
0

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeishauri Wizara ya Maliasili na Utalii iendelee kuzifanyia maboresho kanuni...

RECOMMENDED

Waziri Mwijange aja na orodha ya viwanda visivyofanya kazi

by Patricia Richard
March 23, 2018
0

  Na Mwandishi wetu. Baada ya Rais John Magufuli kuonyesha kukerwa na kitendo cha Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji...

Nane Nane itumike kama darasa huru kwa wakulima

by Patricia Richard
March 23, 2018
0

Na Mwandishi wetu Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) imejitolea kuwapa mafunzo ya siku moja wakulima mkoani Lindi...

No Result
View All Result
  • Home
  • FEDHA
    • MIKOPO
    • BIMA
    • HISA
  • BENKI
  • BIASHARA
    • UJASIRIAMALI
    • UWEKEZAJI
    • BIASHARA NDOGO NDOGO
  • VIWANDA
    • MIUNDOMBINU
    • NISHATI
    • UZALISHAJI
  • KILIMO
    • KILIMO BIASHARA
    • KILIMO UFUNDI
  • MAHOJIANO
  • AFRIKA MASHARIKI
    • BIASHARA
    • FEDHA
    • UJASIRIAMALI

© 2023 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In