Shirika la maendeleo ya petrol nchini TPDC limepongezwa na naibu waziri wa nishati mheshimiwa Subira Mgalu kwa kufanya kazi kwa wakati baada ya kumaliza utoboaji wa bomba la gesi asilia mkoani Pwani.
TPDC kwa kupitia kampuni tanzu ya Gasco ilipewa kazi ya kutoboa bomba hilo la gesi asilia ii kuweka tolea katika kijiji cha mwanambaya katika wilaya ya mkuranga mkoani humo.
Bomba hilo lilitobolewa maalumu ili kuruhusu usambazaji wa gesi asilia kwa wateja mbalimbali wilayani mkuranga kwa lengo la kuvifikia viwanda na wateja wa kawaida ili kupunguza uharibifu wa mazingira hasa kutokana na kukithiri kwa matumizi ya nishati ya kuni na mkaa wilayani humo.
Naye Mhandisi wa mitambo wa kampuni hiyo ya Gasco alisema utoboaji wa bomba hilo umefanywa kitaalamu na umakini wa hali ya juu ili kuepuka athari mbalimbali hasa zinazotokana na harakati za binadamu na mabadiliko ya hali ya hewa.