Home FEDHAMIKOPO Wakulima,wajasiriamali kulamba bilioni 500 NMB

Wakulima,wajasiriamali kulamba bilioni 500 NMB

0 comment 111 views

Mkuu wa kitengo cha wateja wakubwa na serikali wa NMB Filbert Mponzi amesema benki hiyo imetenga kiasi cha Sh. 500 bilioni maalum kwa ajili ya wajasiriamali na sekta ya kilimo na mifugo ili kuchochea ushiriki wa sekta binafsi katika kujenga uchumi. Mponzi amesema hayo katika mkutano mkuu wa 34 wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT) na kuongeza kuwa benki ya NMB imekuwa mstari wa mbele kutekeleza harakati mbalimbali pamoja na serikali ikiwemo kuinua wananchi kiuchumi. Mponzi pia ameweka wazi kuwa fedha hizo zitakopeshwa kwa kipindi cha miaka mitano ili kuwezesha wananchi kushiriki katika ujenzi wa taifa.

“Uchumi wa viwanda unategemea sana sekta ya kilimo na mifugo, hivyo NMB itaendelea kuwa mstari wa mbele kuwasaidia wajasirimali wadogo kupata mikopo nafuu na rafiki ili kuimarisha miradi yao”. Ameeleza Mkuu huyo.

Kwa mujibu wa ripoti ya Benki kuu ya Tanzania (BoT), kwa miaka miwili iliyopita mikopo ya benki za biashara kwenda sekta binafsi imeonyesha kupungua kutokana na kuongezeka kwa mikopo isiyolipika, kulikochangia kushusha faida ya taasisi mbalimbali za kifedha nchini.

Katika maelezo yake, Mponzi pia ametaja sababu iliyopelekea NMB kupandisha bajeti baada ya kukopesha zaidi ya Sh. 280 bilioni kwa miaka miwili iliyopita kuwa ni kuwanufaisha watanzania wengi zaidi.

Leave a Comment

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter