Home VIWANDANISHATI Wananchi Tanga washauriwa kuchangamkia fursa mradi wa gesi

Wananchi Tanga washauriwa kuchangamkia fursa mradi wa gesi

0 comment 100 views

Afisa Mwandamizi kutoka Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) Ayubu Masenza ametoa wito kwa wananchi wa mkoa wa Tanga kuchangamkia fursa ikiwemo kupokea mradi mpya wa bomba la gesi toka Tanga hadi Uganda, mradi ambao utakwenda sambamba na mradi mkubwa wa bomba la mafuta. Masenza amesema hayo alipozungumza na waandishi wa habari wakati wa kilele cha maadhimisho ya siku ya vijana kwenye viwanja vya Tangamano jijini humo.

Masenza amefafanua kuwa mbali na mradi wa bomba la mafuta, serikali ya nchini Uganda ipo katika mchakato wa ujenzi wa mradi wa bomba la gesi litakaloanzia jijini humo hadi nchini Uganda na kuongeza kuwa Tanga itakuwa miongoni mwa majiji ambayo yanakuwa kwa kasi kutokana na uwepo wa miradi mikubwa ambayo inatarajiwa kutekelezwa na serikali za pande zote mbili ikiwa ni matokeo ya ushirikiano mzuri wa kiuchumi.

Aidha, Afisa huyo amedai kuwa uwepo wa gesi jijini Tanga utaongeza fursa za uwekezaji kutokana na viwanda vingi kutumia gesi katika shughuli zake za uzalishaji. Pamoja na hayo, mradhi huo utapelekea ongezeko la ajira na kuchochea kuongezeka kwa matumizi ya gesi hasa viwandani, mashuleni, taasisi za kijeshi, hospitali na kwa wananchi wa kawaida, jambo ambalo linaweza kupunguza uharibifu wa mazingira.

“Ni jukumu la wananchi wa Tanga sasa kuweza kunufaika, mbali na serikali lakini pia mwananchi mmoja mmoja wana nafasi kubwa kunufaika na miradi hii itakayoweza kubadilisha maisha yao kwa ujumla”. Amesema Masenza.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter