Home FEDHA Mkongo wa taifa wa mawasiliano waongeza mapato

Mkongo wa taifa wa mawasiliano waongeza mapato

0 comment 37 views

Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye amesema serikali imefanikiwa kuongeza makusanyo ya mapato kwenye maeneo ya mipakani mwa nchi pamoja na nchi jirani za Uganda, Burundi, Rwanda na Congo kupitia mkongo wa taifa wa mawasiliano. Nditiye amesema hayo wakati akikagua mkongo wa taifa wa mawasiliano kwenye kituo cha mpakani cha Mtukula kinachowezesha usafirishaji wa taarifa na data za wateja na bidhaa kutoka Tanzania kwenda Uganda.

“Maeneo ya mipakani ni lango la kuongeza mapato na kukuza uchumi wa nchi yetu, niwatake muendelee na kasi hii ya ukusanyaji wa mapato ya serikali kwa kutumia kituo cha pamoja cha huduma ambapo tayari kwa kipindi cha miezi mitatu ya mwanzo wa mwaka wa fedha wa 2018/2019, mwezi Julai hadi Septemba, 2018 mapato yameongezeka zaidi ya asilimia 100 kwa mwezi na kufikia asilimia 150”. Amefafanua Naibu huyo.

Kwa upande wake, Afisa Mfawidhi wa forodha wa kituo cha huduma cha pamoja cha Mtukula, Mohammed Shamte amesema katika mwaka wa fedha 2018/2019, wanalenga kukusanya Sh. 15.9 bilioni kwa mwaka ambapo mpaka sasa kuna dalili nzuri za kutimiza lengo hilo kwa kuwa tayari wanakusanya Sh. 1.3 bilioni kwa mwezi, ikiwa ni wastani wa asilimia 110 hadi 150 ya makusanyo kwa mwezi ambayo yanavuka malengo.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter