Home BENKI NMB yazidi kuboresha huduma

NMB yazidi kuboresha huduma

0 comment 111 views

Ofisa Mkuu wa mikopo wa Benki ya NMB Tom Borghols amesema benki hiyo imejipanga kuongeza mawakala wapya wapatao 20,000 ndani ya miaka mitatu ijayo ili kupanua wigo wa wateja na vilevile, kusogeza huduma karibu zaidi na watumiaji. Borghols amesema hayo katika mkutano baina ya benki na klabu za wajasiriamali na kuongeza kuwa, NMB imefikia uamuzi huo kama mkakati wa benki hiyo kuwafikia wananchi wengi zaidi.

“Tutaongeza mawakala kutoka 6,000 waliopo sasa hadi 20,000 ndani ya miaka mitatu ijayo ikiwa ni mkakati wa makusudi wa kupanua wigo wetu na kuwafikia watanzania wengi zaidi”. Ameeleza Ofisa huyo.

Kwa mujibu wa Borghols mbali na kuongeza idadi ya mawakala, NMB pia itawawezesha mawakala hao kuanza kufungua akaunti kwa ajili ya wateja wapya kwani hivi sasa, wananchi wengi hasa walio vijijini hulazimika kufuata matawi ya benki ili kupata huduma hiyo na katika kufanya hivyo wanatumia muda mwingi na gharama kubwa.

Kwa upande wao, baadhi ya wajasiriamali waliohudhuria mkutano huo wameishukuru NMB kwa kushusha riba na kusogeza zaidi huduma huku wakitoa wito kwa benki hiyo kuangalia upya sharti la dhamana ya mikopo linalowataka kukabidhi hati rasmi inayotambulika na kusajiliwa serikalini kabla ya kuchukua mikopo.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter