Home BIASHARA Wafanyabiashara wanaoingiza bidhaa feki waonywa

Wafanyabiashara wanaoingiza bidhaa feki waonywa

0 comment 109 views

Makamu wa Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, amesema serikali itafuatilia wafanyabiashara wanaodaiwa kuingiza bidhaa feki na kuuza kwa gharama ya chini kwani wamekuwa wakisababisha kushusha kwa soko la ndani huku vitendo hivyo vikikatisha tamaa wawekezaji wa ndani pamoja na jitihada za serikali kuhamasisha wawekezaji kuja kuwekeza hapa nchini. Makamu wa Rais ameeleza hayo wakati akizindua kiwanda cha African Dragon kinachotengeneza malighafi ya mabati, wilayani Bagamoyo mkoani Pwani kilichojengwa kwa thamani ya Sh. 11 bilioni.

Katika maelezo yake, Makamu huyo amesema kuwa sekta ya viwanda ndiyo mpango wa serikali wa kuhakikisha nchi inafikia uchumi wa kati kupitia viwanda. Aidha, Samia amesifia mkoa wa Pwani kwa kusheheni viwanda kitaifa huku akiwataka waendelee kujipanga na kuvutia zaidi wawekezaji katika mkoa huo.

“Katika utekelezaji wa uchumi wa viwanda, mtoe ushirikiano kwa wawekezaji ili kuweza kutimiza malengo ya serikali ya kuelekea uchumi wa kati”. Ameshauri kiongozi huyo.

Kwa upande wake, Mkuu wa mkoa wa Pwani, Mhandisi Evarist Ndikilo amesema mkoa huo una takribani viwanda 429 vikiwemo vya kati, vikubwa na vidogo ambavyo vimetengeneza ajira za moja kwa moja zaidi ya 20,000 na serikali imeweza kunufaika na ushuru na kodi zinazolipwa na viwanda hivyo.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter