Home BIASHARABIASHARA NDOGO NDOGO Wafanyabiashara Mabibo kuhamishiwa Simu 2000

Wafanyabiashara Mabibo kuhamishiwa Simu 2000

0 comment 141 views

Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Ubungo Merick Luvinga amesema utaratibu wa soko kuu la ndizi na viazi la Mabibo kuhamia kwenye soko lililopo katika kituo cha mabasi cha Simu 2000 tayari umeandaliwa na utaanza rasmi mwezi huu na kuendelea kwa muda wa miezi sita lengo la kufanya hivyo likiwa ni kupunguza tatizo la msongamano wa magari katika eneo la soko la mabibo.

“Tutaanza kulihamisha soko hilo kidogo kidogo kuanzia mwezi huu kwa kipindi cha miezi sita na tutahakikisha kwamba wafanyabiashara wote watahama bila tatizo lolote baada ya kufikia makubaliano maalum”. Amefafanua Kaimu huyo.

Baadhi ya wafanyabishara kutoka soko la Mabibo wamekuwa na maoni tofauti kuhusu uamuzi huo huku wengine wakimuomba Rais wa Tanzania, Dk. John Magufuli kuingilia kati wakidai eneo la Simu 2000 ni dogo na hawawezi kutosha kwani soko hilo la Mabibo linakadiriwa kuwa na wafanyabishara zaidi ya 4,000 na eneo la Simu 2000 halina uwezo wa kupokea idadi hiyo ya watu.

“Ni bora Rais aingilie kati sakata la sisi kuhamishwa hapa ili azuie mpango huu kwani awali tulipewa taarifa za kuhamia Makaburini ambapo ni pakubwa lakini ghafla tunaambiwa tuhamie soko la Simu 2000 ambalo ni dogo”. Amesema mfanyabishara mmoja

 

 

 

Leave a Comment

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter