Benki ya Amana imetimiza ndoto ya wateja wake kwa kuwawezesha kumiliki viwanja katika maeneo mbalimbali nchini kwa kushirikiana na kampuni inajishughulisha na upimaji viwanja ya Property International Limited.
Viwanja hivyo vimekabidhiwa leo mbele ya waandishi wa habari jijini Dar es salaam ambapo Mkuu wa Biashara wa benki hiyo Munir Rajab alisema mafaniko waliyopata ndani ya miaka mitatu ni mengi ila kubwa ni kuwawezesha wateja zaidi ya 300 kumiliki viwanja vyenye hati halali.
Pia aliongeza kuwa kupitia viwanja hivyo wateja wengi wamefanikiwa kupata mkopo katika benki hiyo hivyo kujijenga kiuchumi huku sharti kubwa la mkopo huo likiwa ni kutanguliza asilimia 20 ya thamani ya kiwanja kama malipo ya awali na kiasi kilichobaki kitalipwa kwa muda usiozidi mwaka mmoja na nusu hadi miaka mitatu.
Benki ya Amana ni moja ya benki inayofanya vizuri nchini kufuatia huduma mbalimbali inazotoa kwa wateja wake hasa mikopo iliyo na riba nafuu.