Home HABARI ZA AFRIKA MASHARIKI Ngirente akaribisha wawekezaji Rwanda

Ngirente akaribisha wawekezaji Rwanda

0 comment 106 views

Baada ya kukutana na kufanya mazungumzo na wawekezaji kutoka sehemu mbalimbali barani Afrika, Waziri Mkuu wa Rwanda, Edouard Ngirente amewataka wawekezaji kuchangamkia fursa mbalimbali za biashara zinazopatikana nchini humo. Ngirente amesema hayo wakati wa kufunga Jukwaa la Uwekezaji Afrika (AIF) lililofanyika Afrika Kusini ambapo alimuwakilisha Rais wa Rwanda Paul Kagame. na kuwashauri wawekezaji kutumia fursa zilizopo Rwanda.

Jukwaa hilo ambalo limeandaliwa na Benki ya Maendeleo Afrika (AfDB) liliwakutanisha pamoja wakuu wa nchi na serikali za Afrika ili kuhamasisha uwekezaji katika sekta za miundombinu, biashara, nishati pamoja na kupanga mikakati ya uwekezaji kwa ujumla.

Baadhi ya miradi ambayo ilitajwa na Waziri Ngirente ni pamoja na hoteli za kisasa za Gold Resort na Karongi, ujenzi wa nyumba za gharama nafuu, Kigali kuwa jiji la ubunifu (KIC) na Gabiro Agro Park Project. Mbali na hayo, Waziri huyo pia alipata nafasi ya kuelezea mikakati iliyowekwa na serikali nchini humo ili kutengeneza mazingira rafiki ya biashara hususani katika sekta ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA).

Kwa mujibu wa takwimu za mwaka jana kutoka Bodi ya Maendeleo Rwanda (RDB), uwekezaji nchini Rwanda umefikia Dola za Marekani 1.041 bilioni ikiwa ni sawa na asilimia 62.26 ya uwekezaji wote.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter