Home BIASHARA Jinsi ya kuandaa mpango wa biashara

Jinsi ya kuandaa mpango wa biashara

0 comment 133 views

Biashara yoyote ile inapaswa kuwa na mpango wa biashara. Mpango wa biashara unasimama kama mwongozo na vilevile unahitajika ili kuwavutia wawekezaji na kuwapa picha halisi ya muelekeo wa biashara yako. Watanzania wengi hawana utaratibu huu. Wengi bado huanzisha biashara kiholela, hali ambayo si salama kama lengo ni kuona biashara yako inafika mbali.

Hivyo basi, Unafahamu namna bora ya kuandaa mpango wako wa biashara? Ni vitu gani havipaswi kukosekana katika mpango huo? Japokuwa kuandaa mpango wa biashara inaweza kuwa ni changamoto kwa walio wengi, hizi ni baadhi ya hatua ambazo unaweza kufuata ili kuandaa mpango wako wa biashara.

  1. Fanya utafiti
  • Ni lazima ufanye utafiti na kuelewa vizuri bidhaa yako, kufahamu soko lako ni nani hasa, kujua ni namna gani unaweza kuwavutia wateja na vilevile kuwashawishi kuendelea kuwa wateja wako wa muda mrefu.
  1. Fahamu lengo la mpango huo
  • Wakati unaandaa mpango wako ni vizuri kufahamu ni nini hasa unalenga kupata kutokana na mpango huo. Kila mfanyabiashara huwa na malengo tofauti. Ni vizuri kuwa na lengo kuanzia mwanzo na kuweka lengo hilo wazi katika mpango wako.
  1. Andaa wasifu wa kampuni
  • Wasifu unahusisha masuala kama historia ya kampuni, huduma zinazopatikana, nani hasa ni wateja wako na vilevile kitu kinachotofautisha biashara yako na nyingine. Ni vizuri kuwa na tovuti ili kuvutia wateja au wawekezaji.
  1. Usiache kitu katika mpango wako
  • Wakati unaandaa mpango wa biashara ni muhimu kutoacha jambo lolote. Hii inasaidia kumuonyesha muwekezaji ni namna gani unatumia na kutengeneza fedha. Ni muhimu kuhusisha masuala kama kodi na matumizi ya fedha katika mpango wako ili kutengeneza picha halisi kwa wawekezaji na wadau wengine.
  1. Kuwa na mkakati wa masoko
  • Mpango mzuri wa biashara lazima uwe na kipengele hiki. Mkakati wa biashara lazima uonyeshe malengo na mbinu za kufanikisha malengo hayo. KIla biashara inadhamiria kupata wateja zaidi, kuweka bidhaa mpya sokoni na kuipeleka biashara mbele kwa ujumla.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter