Home HABARI ZA AFRIKA MASHARIKIUJASIRIAMALI Vijana wajasiriamali washauriwa kuongeza ubunifu

Vijana wajasiriamali washauriwa kuongeza ubunifu

0 comment 77 views

Wawakilishi wa vijana kutoka majukwaa ya vijana wilaya ya Arusha wametoa wito kwa  vijana hapa nchini kuwa wabunifu na kubuni bidhaa zenye uwezo wa kuhimili ushindani uliopo katika soko la pamoja la Afrika Mashariki ili wanufaike na fursa za uwepo wa soko hilo na kulitumia kuboresha maisha yao. Wawakilishi hao wameeleza kuwa, vijana wengi wamekuwa wakifanya jitihada mbalimbali kubuni bidhaa zao lakini changamoto kubwa bado ipo katika ubora wa bidhaa hizo katika kushindana na soko la Afrika Mashariki. 

Kwa upande wake, Mratibu wa shirika la vijana la Initiative for Youth ,Laurent Sabuni ameeleza kuwa watanzania hawapaswi kuwa nyuma katika soko hilo na kuwataka kuungana na kufanya biashara kwa kuvuka mipaka ya nchi na kuzalisha bidhaa bora zenye viwango vya kitaifa na kimataifa.

Naye Afisa Vijana wilaya ya Arusha, Nimfa Ramadhani amesema Tanzania inaelekea katika uchumi wa viwanda, hivyo vijana wanayo nafasi ya kutengeneza bidhaa na kuanzisha viwanda vidogo ili kuendana na kasi ya serikali ya ujenzi wa viwanda.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter