Home HABARI ZA AFRIKA MASHARIKIUJASIRIAMALI Wajasiriamali washauriwa kuthibitisha ubora wa bidhaa zao

Wajasiriamali washauriwa kuthibitisha ubora wa bidhaa zao

0 comment 136 views

Mkuu wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS) Kanda ya kusini, Haji Mussa ametoa wito kwa wajasiriamali kutoka wilayani Nachingwea mkoani Lindi kujenga mazoea ya kudhibitisha bidhaa zao ili kuwa na uhakika wa soko. Haji ametoa ushauri huo wakati wa mafunzo ya wajasiriamali, ikiwa ni muendelezo wa kampeni ya kutoa elimu kwa umma, kampeni ambayo inahusisha wazalishaji wa bidhaa mbalimbali kutoka wilaya za Kanda ya kusini.

Mussa ameongeza kuwa asilimia kubwa ya bidhaa zinazozalishwa na wajasiriamali zipo katika orodha ya viwango ya lazima hivyo mzalishaji anatakiwa kuthibitisha ubora kabla ya kuingiza bidhaa sokoni, ili kuwa na uhakika kuwa bidhaa hizo hazitakuwa na madhara kwa mtumiaji. Mkuu huyo kutoka TBS ameeleza kuwa serikali inatambua umuhimu mkubwa wa wajasiriamali katika kuendeleza sekta ya viwanda, na kupitia shirika hilo, Sh. 100 milioni zimekuwa zikitengwa kila mwaka maalum kwa ajili ya kuwasaidia wajasiriamali.

“Shirika linatoa mafunzo kwa wajasiriamali bure, linapima ubora wa bidhaa bure na kutoa leseni ya kutumia alama ya ubora bure kwa mjasiriamali aliyekidhi vigezo, utaratibu huu ni kwa miaka mitatu baada ya hapo mjasiriamali huanza kuchangia kidogo kidogo, hivyo fursa hii mnapaswa kuitumia kikamilifu”. Amesema Mussa.

Kwa upande wake, Ofisa Biashara Msaidizi wa wilaya ya Nachingwea Stella Martin amesema ili kutatua changamoto ya eneo la uzalishaji, wilaya hiyo tayari imetenga eneo la ekari 49.7 kwa ajili ya viwanda na wajasiriamali.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter