Home KILIMO Malipo ya wakulima wa korosho yafikia Bilioni 222/-

Malipo ya wakulima wa korosho yafikia Bilioni 222/-

0 comment 103 views

Waziri Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa amesema hadi sasa jumla ya Sh. 222 Bilioni tayari zimetolewa na serikali kwa ajili ya wakulima wa korosho na kuwataka wale ambao bado wamesalia kuwa wavumilivu kwani walioanza kulipwa ni wale wenye kilo zisizozidi kilo 1,500 na wale wenye kilo zaidi ya 1,500 na wakati huo huo, serikali inaendelea na uhakiki kisha watalipwa.

”Fedha zipo, hakuna mkulima ambaye atapoteza haki yake wote watalipwa. Tunaendelea na uhakiki kwa wale wenye korosho nyingi ili kubaini kama hawajanunua kangomba.” Ameeleza Majaliwa.

Waziri Mkuu amedai kuwa baadhi ya watu wamekutwa na kilo zaidi ya 1,500 na wameshindwa kuonyesha mashamba yao ya korosho, hali inayoweka wazi kuwa wananunua kupitia kangomba. Majaliwa amesema baadhi ya waliokutwa na korosho nyingi ni vijana wenye umri mdogo ambao hawana uwezo kifedha hivyo serikali imepanga mikakati ya kuwakamata wale. wanaowatuma.

Mbali na hayo, Majaliwa amesema lengo la serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Magufuli ni kuhakikisha wakulima wananufaika kupitia kilimo chao, hivyo biashara ya kangomba itadhibitiwa.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter