Home BIASHARA TRA yapigwa stop kufunga maduka ya wasiolipa kodi

TRA yapigwa stop kufunga maduka ya wasiolipa kodi

0 comment 73 views

Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango ameipiga marufuku Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kufunga maduka pamoja na biashara za watu wasiolipa kodi na badala yake, ameitaka mamlaka hiyo kukaa meza moja na wafanyabiashara ili kujadiliana nao. Waziri Mpango amesema hayo wakati akitoa taarifa ya hali ya uchumi wa taifa na utekelezaji wa bajeti ya serikali katika nusu ya kwanza ya mwaka wa fedha wa 2018/19.

“Utaratibu wa kumfungia biashara mfanyabiashara anayedaiwa kodi ili kumshinikiza alipe sasa usitishwe mara moja, isipokuwa kwa wakwepa kodi sugu na hapo lazima kuwe na kibali cha Kamishna wa mkuu wa TRA, nataka mjikite katika kutoa elimu siyo vitisho”. Amesema Dk. Mpango.

Aidha, Waziri huyo ameeleza kutofurahishwa na matumizi mabaya ya lugha, vitisho na ubabe wanavyokumbana navyo walipa kodi wenye historia nzuri na kuonya kuwa, mtumishi wa TRA atakayekiuka taratibu za kiutumishi awajibishwe. Dk Mpango pia ametumia nafasi hiyo kuikumbusha mamlaka hiyo kuwa hata Rais Magufuli amekwishaagiza utaratibu wa kufungia maduka usitishwe wakati akifungua kikao kazi cha TRA Desemba 10, hivyo mamlaka hiyo inapaswa kutekeleza amri hiyo.

Badala ya kufunga biashara za wasiolipa kodi, Waziri huyo ameagiza TRA kujikita zaidi katika kutoa elimu kwa wafanyabiashara ili wafahamu umuhimu na thamani ya kulipa kodi kwa maendeleo ya nchi yao.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter