Home BENKI Bank M kuwa sehemu ya Azania bank Limited.

Bank M kuwa sehemu ya Azania bank Limited.

0 comment 129 views

Benki kuu ya Tanzania(BoT) imekamilisha mchakato wa kuihamisha iliyokua benki M ya nchini Tanzania kuwa sehemu ya benki ya Azania Limited baada ya benki hiyo kupungukiwa ukwasi.

Akizungumza na waandishi wa habari jiji dar es salaam naibu gavana wa benki kuu Dk Bernad kibese alisema uamuzi huo umezingatia kifungu cha 59(4) cha sheria ya mabenki na taasisi za fedha ya mwaka 2006 inachoipa mamlaka benki kuu ya kusimamia taasisi za fedha nchini ambapo baada ya kukamilika kwa mchakato huo sasa rasmi mali na madeni ya benki M yatahamishiwa benki ya Azania.

“Hivyo kwa mamlaka niliyopewa chini ya kifungu cha 58 ibara ya 20(h) cha sheria ya mabenki na taasisi za fedha ya mwaka 2006,benki kuu imeamua rasmi kuhamisha kwa mujibu wa sheria mali na madeni yote ya benki M kwenda Azania benki.

Pia naibu gavana aliwataka wateja wenye amana na wadaiwa wa benki M kuwasiliana na benki kuu huku wakisubiri kuambiwa tarehe rasmi ya kuanza kupata huduma kupitia benki ya Azania huku waliokuwa wateja wa mikopo wakitakiwa kuendelea kurejesha mikopo yao kama walikubaliana na benki M.

Benki M ilipewa leseni hapa nchini mwaka 2008 ikiwa na mtaji wa Trilioni 1 na matawi matano.Bot iliamua kuiweaka katika ungalizi maalumu toka mwezi novemba 2018 baada ya kupungukuwa ukwasi.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter