Home KILIMO Watendaji wazembe sekta ya kilimo wapewa onyo

Watendaji wazembe sekta ya kilimo wapewa onyo

0 comment 113 views

Waziri wa Kilimo Japhet Hasunga amekemea tabia ya uzembe, urasimu na kutowajibika kwa baadhi ya watendaji wa sekta hiyo, hali inayopelekea kucheleshwa kwa pembejeo za kilimo. Waziri Hasunga amesema hayo katika ziara yake ya kukagua shughuli za kilimo mkoani Tabora na kusisitiza kuwa, hali hiyo inakwamisha dhamira ya kuleta mageuzi katika sekta ya kilimo.

“Nisingependa kusikia hadithi za ucheleweshaji wa mbolea zikiendelea huku wakulima wakiendelea kuathirika na hali hiyo, ni lazima sasa tuache kufanya kazi kwa mazoea na kuwasaidi wakulima wafikie malengo ya kuwa na kilimo chenye tija na uhakika”. Amesema Waziri huyo.

Aidha, Hasunga amewtaka watendaji kuwa wabunifu ili kuhakikisha masoko mapya yanapatikana na wakulima wanapata nafasi ya kuuza bidhaa zao kwani kumekuwa na changamoto kubwa hususani kwa zao la tumbaku.

“Tusingependa kusikia kwamba tumbaku haijanunuliwa na ikifikia hapo serikali tutachukua hatua kama tulivyofanya katika zao la korosho, hata hivyo tusingependa tufike huko. Hakikisheni tumbaku yote inanunuliwa mwaka huu. Watendaji wazembe ni vyema wakatupisha kwa kuwa kilimo sio suala la dharura na kina mahitaji ya kila mwaka, hakuna sababu ya msimu ufike ndipo tuanze kushughulika na wakulima, hilo sitalivumilia”.  Amesisitiza Waziri Hasunga.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter