Home VIWANDANISHATI Serikali yatoa VAT umeme Zanzibar, yafuta deni la Bilioni 22

Serikali yatoa VAT umeme Zanzibar, yafuta deni la Bilioni 22

0 comment 74 views

Serikali imeridhia utozwaji wa kodi ya ongezeko la thamani (VAT) kwa kiwango cha asilimia sifuri kwenye umeme unaouzwa na Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) kwa Shirika la Umeme la Zanzibar (ZECO). Aidha serikali imefuta malimbikizo ya deni la Sh. 22.9 bilioni ambayo ni kodi ya VAT kwenye umeme uliouzwa ZECO.

Akizungumza baada ya kikao cha Baraza la Mawaziri ambacho kilihudhuriwa na Rais wa Tanzania Dk. John Magufuli, Makamu wa Rais Samia Suluhu, Rais wa Zanzibar Dk. Ali Mohamed Shein, Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi John Kijazi pamoja na mawaziri, Rais Magufuli amesema baada ya uamuzi huo, Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Philip Mpango atawasilisha marekebisho madogo ya Sheria ya VAT, ili umeme unaokwenda Zanzibar usitozwe kodi.

“Kwa hiyo madeni yatakayokuwa yanadaiwa kwa Zanzibar ni yale madeni ya kulipa umeme, umeme wametumia kiasi fulani wanalipa kama wanavyolipa kwa maeneo mengine mfano Dar es salaam, suala la kutoza VAT sasa halipo na katika hilo kwa sababu kulikuwa na deni ambalo lilikuwa limefikia Sh. 22.9 bilioni, sisi Baraza la Mawaziri tutapeleka mapendekezo Bungeni kwamba lisamehewe kwa sababu lipo ndani ya bajeti ya mwaka huu wa 2018/2019, kwa hivyo litapunguza mapato yatakayotakiwa kukusanywa na serikali”. Amesema Rais Magufuli.

Naye Dk. Shein amesema mbali na kuridhia utozwaji wa VAT kuwa kwa kiwango cha asilimia sifuri, Baraza la Mawaziri pia limekubaliana kuwa Makamu wa Rais ataitisha vikao vya kujadili masuala la muungano kila kunapokuwa na hoja.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter