Home BENKI Wateja CRDB watoa neno

Wateja CRDB watoa neno

0 comment 113 views

Wateja wa benki ya CRDB jijini Mwanza wametoa wito kwa benki hiyo kuboresha huduma zake na kuhakikisha zinawafikia hata wale walio katika maeneo ya vijijini kwa kuwapatia mikopo iliyo na riba nafuu.

Hayo yamesemwa wakati wa hafla ya kumtambulisha rasmi Mkurugenzi Mtendaji mpya ya CRDB, Abdulmajid Nsekela kwa wateja wa benki hiyo mkoani humo. Hafla hiyo iliandaliwa na CRDB ikiwa na dhumuni la kuwainua wajasiriamali na kusaidia mzunguko wao wa fedha.

Katika maelezo yake, Nsekela amesema jiji la Mwanza ni kitovu cha kukuza uchumi hapa nchini na kuongeza kuwa, benki ya CRDB inatambua mchango wa mkoa huo kwa wateja wao. Aidha, Mkurugenzi huyo ameongeza kuwa, benki hiyo ina matawi takribani 265, mitandao isiyopungua 550 na vilevile inatoa huduma kupitia mawakala zaidi ya 5,000.

Nsekela pia ameeleza kuwa, benki hiyo inaendelea kupanua wigo wake wa utoaji huduma kwa wananchi na imeanzisha kampuni tatu ikiwemo moja ya kutoa huduma ya bima kwa wananchi.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter