Home BENKI Wakulima, wafugaji walamba bilioni 500

Wakulima, wafugaji walamba bilioni 500

0 comment 121 views

Benki ya NMB imetoa bilioni 500 kwa wafugaji na wakulima wa viwanda vidogo na vikubwa nchini ili kuleta maendeleo zaidi katika sekta hizo. Meneja Mwandamizi Idara ya Mikopo na Kilimo, Isack Nyangaro, amesema kuwa dhumuni la kutoa pesa hizo ni kutimiza azma ya serikali ya awamu ya tano ambayo imejikita katika kukuza uchumi kupitia sekta ya viwanda.

Waziri wa Mifugo Luhaga Mpina, amesema kuwa hadi sasa, Kenya inazalisha maziwa lita bilioni 5.2, wakati Tanzania inazalisha lita bilioni 2.4 pekee, jambo ambalo haliridhishi hasa kutokana na Tanzania kuwa na hali nzuri ya hewa kuliko Kenya. Waziri huyo ametoa wito kwa wafugaji kuongeza juhudi ambayo itawapelekea kupata soko zaidi.

Aidha, Waziri Mpina amezitaka benki na taasisi za fedha kwa ujumla kuendelea kuwapatia mikopo wafugaji ili waweze kuzalisha zaidi. Hadi sasa, serikali imefanikiwa kufunga mitambo ya kugundua magonjwa ya mifugo na namna ya kutibu mifugo hiyo hivyo, Waziri Mpina amewahakikishia wafugaji kuwa ndani ya mwaka mmoja, chanjo zote kumi na moja zitakuwa zikipatikana nchini ili kuwawezesha wafugaji kufanya ufugaji wa kisasa.

“Tunadhibiti kuhakikisha hakuna chanjo isiyo salama kwa mifugo yetu lengo ni kusonga mbele katika ufugaji”. Amesema Mpina.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter