Home BENKI Mikoa inayoongoza kuchafua noti yatajwa

Mikoa inayoongoza kuchafua noti yatajwa

0 comment 116 views

Mikoa ya Kagera na Kigoma imeanza kuelimishwa na Benki kuu ya Tanzania (BoT) kuhusu matunzo ya fedha na sehemu husika ya kupeleka fedha chakavu. Meneja Msaidizi wa Uhusiano kwa Umma BoT,Victoria Msina ametaja mikoa hiyo kuwa vinara wa noti mbovu na chakavu kuwataka wananchi kuwa na utaratibu wa kwenda kubadilisha fedha chakavu kwenye matawi ya benki za kibiashara.

“Utafiti tuliofanya tumebaini mikoa ya Kigoma na Kagera inaongoza kwa kuchafua noti . Fedha zinachakaa mno ukilinganisha na mikoa mingine, ndiyo maana tumeanza kutoa elimu kuanzia na mikoa hiyo miwili” Amesema Meneja Msaidizi huyo.

Diwani wa Kigoma Mjini, Hussein Kalyago, amesema kuna umuhimu mkubwa wa BoT kutoa elimu kwa wananchi kuhusu matunzo ya fedha akieleza kuwa wananchi wa Kigoma wamekuwa wakishindwa kutumia noti zao mikoa mingine kutokana na uchakavu wa noti hizo.

Naye Meneja Msaidizi wa Utunzaji Fedha na Alama za Usalama BoT, Abdul Dollah ametoa wito kwa wananchi kuacha tabia ya kuuza noti chakavu kwa wale wanaonunua kwa gharama ndogo na kuwataka wananchi hao kupeleka fedha hizo kwenye benki za biashara.

“Benki zote sasa zinapokea fedha mbovu na chakavu na utabadilishiwa kwa kupewa fedha nzima bila kukatwa, lengo ni kupunguza usumbufu unaojitokeza”. Amesema Dollah.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter