Home VIWANDA Ndalichako asisitiza ubunifu kufikia uchumi wa viwanda

Ndalichako asisitiza ubunifu kufikia uchumi wa viwanda

0 comment 119 views

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Joyce Ndalichako ametoa wito kwa wanafunzi wanaojikita katika masomo ya sayansi, pamoja na wabunifu hapa nchini kubuni vitu ambavyo vitasaidia kurahisisha shughuli mbalimbali zinazofanywa na wananchi. Ndalichako amesema hayo katika kilele cha Mashindano ya Sayansi, Teknolojia na Ubunifu  (MAKISATU) jijini Dodoma. Mashindano hayo yalibeba kaulimbiu ya ‘Kukuza ujuzi na ubunifu kwa uchumi wa viwanda’.

“Changamoto tuliyonayo kwa sasa ni muamko kwa wananchi haujafikia katika kiwango ambacho serikali ingependa kukiona, ni wazi kabisa tunapaswa kuwa na ubunifu na kutumia sayansi na teknolojia kuhakikisha tunarahisisha maisha ya wananchi wanaoishi vijijini. Ninatoa wito kwa wabunifu wote nchini kuhakikisha wanajikita kuangalia ni kwa namna gani wanarahisisha shughuli zinazofanyika katika mazingira yao na ikumbukwe ubunifu hauna umri na hauchagui kwa sababu mwisho wa siku mkono unaenda kinywani”. Amesema Ndalichako.

Naye Kaimu Katibu Mkuu, Prof. James Mdoe amesema mashindano hayo ambayo yanahusisha wabunifu kutoka ngazi mbalimbali za elimu yanalenga kuibua ubunifu, umahiri na kuchochea ugunduzi ili kukuza matumizi ya sayansi na teknolojia katika kuleta maendeleo.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter