Home KILIMO Kilio cha wakulima korosho kusikilizwa

Kilio cha wakulima korosho kusikilizwa

0 comment 115 views

Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar, Zuberi Maulidi, ameahidi kuwasilisha kwa Rais Magufuli changamoto wanazokumbana nazo wakulima wa korosho. Spika huyo ambaye pia ni Mlezi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) mikoa ya Lindi na Mtwara amewahakikishia hayo wakulima wakati wa ziara yake ya kukagua shughuli mbalimbali za maendeleo baada ya kuelezwa kuwa wakulima wamerudishiwa zaidi ya tani 160 za korosho katika vyama vya msingi vya Mtungulu na Lengo wilayani Newala.

“Niwaahidi na niwahakikishieni kuwa malalamiko yenu nimeyapata kwa ukamilifu na ninaahidi kuyafikisha kwa Mwenyekiti wetu wa taifa (Rais John Pombe Magufuli) na naahidi kwamba nikitoka hapa nakwenda kuyafikisha na nataka nimfikishie kwa mkono wangu na kumhadithia kwa mdomo hali niliyoikuta”. Amesema Spika Maulidi.

Spika huyo ameonyesha kutopendezwa na wakulima kurudishiwa korosho hizo bila malipo ikiwa wameshapewa stakabadhi ya malipo hapo awali. Ameeleza kuwa kuna umuhimu mkubwa wa kufuatilia changamoto hizo kwa kina kwani korosho ni zao muhimu sana na kupitia zao hilo, uchumi unaendelea.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter