Home VIWANDANISHATI “KA-TA” yaingizia TANESCO bilioni 41

“KA-TA” yaingizia TANESCO bilioni 41

0 comment 147 views
Na Mwandishi wetu

Meneja Mwandamizi Hesabu wa TANESCO Philidon Siyame amewaambia waandishi wa habari kuwa shirika la umeme (TANESCO), chini ya utendaji wa serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais Magufuli shirika hilo limefanikiwa kukusanya Sh bilioni 41 ndani ya miezi mitano kutoka kwa wadaiwa sugu katika asasi za serikali na watu binafsi.

Ameongeza kuwa Machi mwaka huu deni lilikuwa Sh 275 bilioni ambapo Shirika la Umeme Zanzaibar (ZECO) walikuwa wakidaiwa Sh 180 bilioni ambapo hadi kufikia sasa wamelipa Sh 18 bilioni. Kutoka taasisi za serikali karibuni Sh 18 bilioni zimepatikana huku madeni ya watu binafsi yaliyolipwa mpaka sasa ni Sh 5 bilioni.

Hapo awali haikuwa rahisi kukusanya madeni lakini tangu Rais John Magufuli alipoanzisha kampeni ya “KA-TA” TANESCO imefanikiwa kwa kiasi kikubwa kufanya hivyo na kupelekea uwezo wa kukusanya mapato wa shirika hilo kufikia hadi asilimia 104 kutoka asilimia 90.

Kupitia Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyakazi wa Viwanda na Biashara(TUICO) wa shirika hilo. Bw. Hassan Athumani, TANESCO amesema inashukuru na kumpongeza Rais kwa utendaji wake katika kufanikisha kuwa wadaiwa sugu wote wanalipa madeni yao.

 

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter