Home KILIMO Tari yawekeza elimu, teknolojia sekta ya kilimo

Tari yawekeza elimu, teknolojia sekta ya kilimo

0 comment 151 views

Mkurugenzi wa Kituo cha Utafiti wa Kilimo (Tari), Dk. Tulole Bucheyeki amesema ili kufikia uchumi wa viwanda, serikali imewekeza katika elimu na teknolojia za kisasa kwenye sekta ya kilimo ili kuongeza uzalishaji wa mazao ya chakula na biashara hususani kwa wakulima wadogo.

“Tumeamua kuwekeza elimu na ujuzi kwa wakulima wadogo ili kuongeza uzalishaji hasa wa mazao kwa lengo la kuweka usalama wa chakula kwa taifa letu, tunatambua kuwa serikali ina sera ya taifa ya kuelekea kwenye uchumi wa viwanda, hii itasababisha vijana wengi kwenda kufanya kazi viwandani hivyo wale wachache wataobaki kwenye kilimo ni lazima wawe na elimu na ujuzi ili wazalishe chakula cha kukidhi mahitaji ya taifa”.Ameeleza Mkurugenzi huyo.

Dk. Bucheyeki amesema ili kukidhi mahitaji ya chakula na malighafi za viwandani zinazotokana na kilimo, wakulima wanatakiwa kupata elimu ya kutosha kuhusu kilimo cha kisasa ili kukidhi mahitaji.

Naye Katibu Tawala Msaidizi masuala ya uchumi na uzalishaji mkoani Songwe, Vanciar Kulanga amesema kupitia kilimo biashara, wakulima watanufaika kiuchumi. Ameshauri wakulima kuwa na kumbukumbu za taarifa kuhusu uzalishaji ili iwe rahisi kwa serikali kuwatafutia masoko.

“Lipo tatizo la kutokuwapo kwa taarifa za kiasi cha mazao yaliyozalishwa mkoani Songwe, hii inasababisha serikali kutokuwa na takwimu sahihi za mazao ya ziada yaliyopo kwa wakulima na hivyo kushindwa kuwatafutia soko la mazao yenu”. Amesema Kulanga.

 

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter