Home HABARI ZA AFRIKA MASHARIKIUJASIRIAMALI Unachotakiwa kufahamu kuhusu biashara ya kuku    

Unachotakiwa kufahamu kuhusu biashara ya kuku    

0 comment 201 views

Biashara ya kuku ni moja kati ya biashara maarufu zaidi hapa nchini. Umaarufu wake umetokana na ukweli kwamba, mtaji unaohitajika kuanzisha biashara hii ni kidogo tu. Mbali na mtaji, unapoanzisha biashara hii inabidi uwe mvumilivu na mwenye kujituma kwa sababu faida inaweza isipatikane mara moja. Watu wengi wamefanikiwa kupitia biashara hii.

Yafuatayo ni mambo machache ambayo mfanyabiashara anayefikiria kuwekeza katika mradi wa kuku anatakiwa kufahamu:

Mfanyabiashara anatakiwa kujua kama anataka kufuga kuku wa kisasa au wa kienyeji. Kuku hufugwa kwa kipindi kifupi hivyo mfugaji anaweza kurudisha mtaji na faida baada ya muda mfupi. Kwa kawaida, kuku  wa kienyeji hawana magonjwa mengi na hata wale kuku wa kisasa kwa mfano aina ya sasso humfikia mfugaji tayari wakiwa wamepata chanjo hivyo mfugaji anabaki na jukumu la kuhakikisha mazingira ni salama.

Tambua kuwa unaweza kufanya biashara mbalimbali kupitia kuku, kwa mfano unaweza kuuza kuku wenyewe, unaweza kuuza mayai, unaweza kuuza nyama, unaweza kuzalisha chakula cha kuku na kuuza na unaweza kupata mbolea na kuuza. Fanya utafiti ili kujua biashara gani ya kuku itakupa faida zaidi.

Kama lengo lako ni kufuga kisha uuze kuku hao, inafaa kufahamu wapi unataka kufanya ufugaji huo kama huna eneo basi tafuta eneo la kufugia. Kuna mabanda madogo, ya kati na makubwa hivyo fanya fahamu bei na gharama zitakazohitajika. Hakikisha hutumii gharama kubwa sana kuandaa sehemu ya kuwafugia kuku hao. Pia hakikisha banda lako sio kero majirani au watu walio karibu endapo utafuga kwenye maeneo yenye watu wengi.

Pata ushauri kutoka kwa wataalamu. Kuna njia ya kufuga ndani na kuwaacha huru kuku wakati wa mchana. Njia ya kuwaacha huru ni nzuri lakini changamoto zake ni magonjwa, wezi, pia ni ngumu kufuatilia ukuaji wa kuku wako. Kufugia ndani ni salama na rahisi kufuatilia ukuaji ingawa ni hatari kwani kuku wanaweza kuambukiza magonjwa. Mtaalamu anaweza kukushauri jinsi ya kujenga banda lako na kuku wakapata hayo yote kwa pamoja.

Vilevile, unatakiwa kufahamu kuhusu vifaa. Vipo vifaa vingi vinavyohitajika katika ufugaji wa kuku na vinategemea na kuku utakaofuga. Baadhi ya vifaa vya kuku ni vifaa kwa jili ya kula, taa, inkubeta, kreti, mfumo wa kutoa taka bandani, hita, viota na penchi.

Pia unatakiwa kujua namna ya kulisha kuku wako. Ukifanya utafiti inakuwa rahisi kuamua kama utatengeneza mwenyewe chakula au utakuwa unanunua. Jambo la kuzingatia ni kupata chakula hicho kwa bei nafuu. Ukiamua kutengeneza na faida inaongezeka zaidi kwa sababu utaweza kuwauzia wafugaji wengine. Na ukipata faida basi ni rahisi kuipanua zaidi biashara yako.

Ni muhimu kuwa na mtaalamu atakayekuwa anakuja kuangalia afya za kuku wako. Hii itasaidia sana katika kudhibiti magonjwa na kuwapatia chanjo. Pia ni muhimu wewe kama mfugaji kuhudhuria katika maonyesho na semina mbalimbali ya kuku na ufugajii kwa ujumla ili kujifunza zaidi kutoka kwa wengine na kutangaza biashara yako.

 

Leave a Comment

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter