Home BENKI Benki zaonywa uhamishaji fedha za Deci

Benki zaonywa uhamishaji fedha za Deci

0 comment 110 views

Baada ya Mahakama Kuu Kanda ya Dar es salaam kuamuru fedha za taasisi ya Development Entrepreneurship for Community Initiative (Deci) pamoja na mali kutaifishwa na serikali, Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) Biswalo Mganga ametoa onyo kwa benki zenye akaunti za fedha hizo kutozihamisha kwani hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yao.

Mganga amewaambia waandishi wa habari kuwa kutokana na uzoefu uliojitokeza mwaka huu ambapo taasisi ya upatu ya Rifaro iliagizwa na mahakama kutaifisha mali zake zikiwemo Sh. 149 milioni, amelazimika kutoa onyo hilo.

“Natoa hii kama tahadhari kwa bank managers (mameneja wa benki) wote ambako fedha hizi zipo wasifanye mchezo wa kuhamisha kuzipeleka sehemu nyingine yoyote ile, aidha kwa kurubuniwa kwa njia ya rushwa au ya nini vinginevyo watapata mambo yatakayowapata mahakamani. Ninafahamu bado kuna watanzania ambao wanaendelea kujiingiza kwenye upatu. Nawaomba waache. Tumeanza na Deci 2009 tukaja Rifaro ambayo fedha zake zimeshataifishwa, kote huko wataendelea kupoteza fedha”. Amesisitiza DPP.

Siku chache zilizopita, Jaji Stephen Magoiga aliagiza mameneja wa benki za NMB Msasani, Dar es salaam Community Bank (DCB) tawi la Uhuru pamoja na Kenya Commercial Bank (KCB) Samora Avenue kuhakikisha fedha hizo zinafika serikalini baadha ya kuridhia kuwa zilizalishwa kutokana na uhalifu wa kuendesha shughuli za upatu kinyume na Sheria.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter