Home HABARI ZA AFRIKA MASHARIKIFEDHA Bilioni 52 zakusanywa Iringa

Bilioni 52 zakusanywa Iringa

0 comment 134 views

Ofisa Mwandamizi huduma na elimu kwa mlipa kodi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) mkoani Iringa Barnabas Masika amesema mkoa huo umefanikiwa kukusanya Sh. bilioni 52.888 ambazo ni sawa na asilimia 87 kwa mwaka wa fedha 2017/18.

Masika amesema kuwa mkoa huo ulikuwa na malengo ya kukusanya bilioni 60.734 kwa mwaka wa fedha 2017/18, na kwa mwaka wa fedha 2018/19 wamelenga kukusanya mapato ya Sh. bilioni 60.393. Ofisa huyo ameeleza kuwa kuanzia Julai mwaka jana hadi Aprili mwaka huu, wamefanikiwa kukusanya bilioni 48.907 ambayo ni asilimia 99.8.

Pamoja na hayo, Masika ameongeza kuwa wanafanya kila jitihada kuhakikisha wanafikia malengo ya mkoa ikiwa ni pamoja na kuboresha huduma kwa kutoa elimu kuhusu kodi kwa wananchi kwa ujumla, kuendeleza ushirikiano kwa wadau mbalimbali, kufuatilia matumizi ya mashine za kodi za kielektroniki (EFD) na kuongeza wigo wa kodi ikiwa ni pamoja na kutafuta vyanzo vya mapato.

Kwa upande wake, Naibu Mkurugenzi wa rasilimali watu na utawala bora Alice Lukindo amewasisitiza wafanyabiashara kutoa risiti na wateja kuomba risiti pindi wanaponunua bidhaa.

“Ndugu zangu kuna baadhi ya wafanyabiashara hawatoi risiti kwa wateja wao hilo ni kosa la jinai na sisi kama TRA tukimkamata mfanyabiashara kama huyo tutamshughulikia kama sheria inavyotaka na nyinyi wanunuzi pendeni kuchukua risiti kwa sababu ni  haki yenu”. Amesema Naibu huyo.

 

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter