Home FEDHA Faida na hasara za kubeti

Faida na hasara za kubeti

0 comment 261 views

Kubeti kwa kifupi ni kubashiri au kuotea kwa mfano kwenye michezo kama mpira kuwa timu fulani watashinda au kushindwa. Mtu anayebashiri huweka fedha kiasi fulani na ikiwa ubashiri wake utakuwa sahihi basi hushinda fedha zaidi ya zile alizoweka. Kubeti kunaweza kumletea mtu fedha nyingi au hasara moja kwa moja. Hivyo ni muhimu kwa mashabiki wa kubeti kuwa makini na kustahimili hasara.

Kutokana na utandawazi, siku hizi watu wanaweza kubeti kwa kupitia simu za mkononi, kwenye kampuni husika pamoja na sehemu za kasino. Hapa kwetu, kuna makampuni mengi yanaendesha shughuli hii ya kubeti. Baadhi ya makampuni yanayofahamika ni pamoja na Mkekabet, Meridianbet, SportsPesa na Premier Bet.

Faida:

Uwezekano wa kushinda fedha nyingi na kutajirika. Kila siku watu wanajishindia mamilioni ya fedha kupitia kubeti hivyo kubadilisha maisha yao. Mara nyingi wenye uwezo mkubwa wa kushinda fedha nyingi ni wale wanaowekeza kiasi kikubwa ndio maana ukiwa unabeti unatakiwa kuwa tayari kupata faida au hasara hasa kutokana na kiasi cha fedha utakachoweka wakati unabeti.

Watu hubeti, kwa ajili ya kujifurahisha. Ikiwa mhusika atashinda basi hata furaha yake huongezeka. Kuna watu hufurahia tu kitendo cha kusubiria, ile hofu ya kupata au kukosa huwafurahisha baadhi ya watu hivyo hata akishindwa huwa si tatizo kwao na wakishinda basi furaha huongezeka.

Ili kubeti sio lazima uwe na ujuzi kuhusu kubeti. Kuna watu wamekuwa wakibeti muda mrefu lakini hawajabahatika kushinda kiasi kikubwa cha fedha na kuna watu wamebeti mara mbili tatu na kujishindia kiasi kikubwa cha fedha.

Hasara:

Uwezo wa kupoteza fedha nyingi. Watu hupoteza fedha nyingi bila kujua kupitia kubeti. Mara nyingi mashabiki wa mchezo huu huendelea kubeti hasa wakiona watu wengine wanapata fedha au wakiona wameshinda mara ya kwanza basi watataka waendelee kubeti ili washinde zaidi, hivyo kupelekea kutumia fedha nyingi kwa mantiki kwamba watashinda tena.

Kuna watu wanashindwa kuacha kubeti watu hawa hata wajitahidi vipi, inashindikana kuacha kubeti kwa sababu akili yao imeshatawaliwa na mchezo huu (Addiction) na ikifika hatua kwamba huwezi kuishi bila kubeti basi hilo ni tatizo kubwa sana kwa sababu fedha nyingi sana zitaelekezwa katika kubeti hivyo kusababisha kufilisika, biashara kufa, ukosefu wa mahitaji n.k. Watu wengi wameathiriwa na mchezo huu hivyo kuharibu maisha yao kwa ujumla. Ni muhimu kucheza mchezo huu kwa mpangilio.

Watu wenye makampuni yanayohusu na kubeti, wamelenga kupata faida nyingi, hivyo kabla hujaanza kucheza unashauriwa kujua kwamba mfanyabiashara wa kubeti hufaidia zaidi yako hivyo fanya maamuzi sahihi. Kama unataka kujifurahisha basi sio vibaya kubeti lakini kama unabeti kwa lengo la kuwekeza ni muhimu kutafakari kwa kina kwani uwezo wa kushinda ni mdogo wakati ule wa kushindwa ni mkubwa zaidi.

Leave a Comment

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter