Home FEDHA Vikwazo vikubwa vya mafanikio

Vikwazo vikubwa vya mafanikio

0 comment 119 views

Watu wanafanya kazi kwa bidii ili wawekeze zaidi na kuongeza kipato. Lakini kufanya kazi kwa bidii peke yake haimaanishi kwamba utafanikiwa zaidi hasa kama hujajiwekea mipango mathubuti itakayosaidia kuongeza fedha zaidi.

Hivyo ikiwa unayafanya haya basi itakuwa ngumu kwako kufanikiwa katika maisha:

Kutokuweka akiba

Akiba ni muhimu sana kwa kila mtu, kwasababu kupitia akiba unaweza kusuluhisha matatizo ya gafla, kupitia akiba unaweza kutatua matatizo ya gafla katika biashara au kampuni yako. Ndiyo maana watu hushauriwa kutumia fedha katika vitu vya muhimu, na kupunguza matumizi kwenye mambo ya anasa. Si vibaya kujifurahisha na anasa mara moja moja lakini usiwekee kipaumbele vitu ambavyo unajua huna uwezo nao kwa kufanya hivyo itakuwa rahisi kujiwekea akiba na kufanya mambo ya kimaendeleo.

Kupuuza fursa zinazojitokeza

Kuna watu ambao hupuuza fursa kutokana na sababu mbalimbali moja wapo ikiwa ni uoga. Kila kitu si rahisi hivyo hata mabadiliko pia huwa yanaogopesha lakini ukipata mafanikio utajishukuru kwa kuamua kuchukua hatua ulizochukua. Hivyo basi kama unaona unaweza kumuinua mtu kwa kuwekeza basi fanya hivyo, na ikiwa umepata mtu anayetaka kubadilisha mwenendo wa biashara au kampuni basi usipuuzie, tafakari kwa makini fanya maamuzi kwaajili ya maendeleo makubwa zaidi.

Kutokufanyia kazi mawazo yenye maana

Ni kawaida kusikia watu wanaongelea mawazo waliyonayo kuhusu masuala ya uchumi na fedha. Wazo peke yake haliwezi kuweka fedha katika akaunti yako, matendo yatafanya wazo libadilishe mwenendo wa uchumi wako hivyo kama una mawazo yanayoleta maana acha kupoteza muda kwa kuwaelezea watu, anza kuyatendea kazi na kuyafanya yawe katika uhalisia. Pia kumbuka kuwa hata mabilionea unaowajua nao walianza kuwaza kwanza, na baadae wakatenda ili kuleta uhalisia wa fikra zao na ndio maana wamefanikiwa.

Kufanya maamuzi kwa kutumia hisia

Maamuzi yanayofanywa na hisia mara nyingi huleta matatizo zaidi. Hivyo weka pembeni hisia zako ukiwa kazini, katika biashara yako, au kampuni ili kufanya maamuzi sahihi. Kutokufanya hivyo kutakurudisha nyuma kimaendeleo. La muhimu zaidi, ni kufikiria kwanza kabla ya kutenda au kutamka. Kwa sababu kila unachokifanya au kutenda kinaweza kuleta mwisho mzuri au mbaya.

Leave a Comment

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter