Home BENKI Exim yatoa milioni 2OO kuboresha sekta ya afya

Exim yatoa milioni 2OO kuboresha sekta ya afya

0 comment 135 views
Na Mwandishi wetu

Katika kusherekea miaka 20 ya uvumbuzi na kujitolea kwa jamii, Benki ya Exim imezindua mradi unaojulikana kama ‘Miaka 20 ya kujali jamii’ na kuwekeza kiasi cha Sh milioni 200 kwenye sekta ya afya huku mradi huo ukilenga kupunguza tatizo la ukosefu wa vitanda vya kutosha katika hospitali kote nchini.

Katika hafla ya kuadhimisha miaka 20 ya benki hiyo ambayo ilifanyika katika Hospitali ya Temeke, Mkuu wa kitengo cha fedha cha benki hiyo Selemani Ponda amesema kwa miaka mingi sasa benki hiyo imekuwa ikiwekeza katika sekta za afya, mazingira na elimu. Ameongeza kuwa kwa kuona jitihada mbalimbali zinazofanywa na serikali ili kuboresha sekta ya afya hapa nchini, benki hiyo imejitolea kuwekeza katika hospitali za serikali kote nchini kwa kipindi cha mwaka mmoja.

Dk. Gwamaka Mwabulambo, Mganga Mkuu wa hospitali ya Temeke ambayo ni mmoja wa wanufaika katika mradi huu amesema msaada huo ni muhimu sana kwa hospitali hiyo kwani kuna changamoto kubwa ya upungufu wa vitanda.

Mradi huu unategemea kutoa magodoro 500 pamoja na vitanda katika hospitali za serikali kwenye mikoa 13 kote nchini.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter