Home BENKI Online Banking: Faida na hasara zake

Online Banking: Faida na hasara zake

0 comment 125 views

Benki mbalimbali zinafanya kila jitihada kurahisisha huduma zao kwa wateja. Huduma za kibenki mtandaoni ni moja ya huduma ambayo wateja wengi katika benki mbalimbali wanaifurahia hasa kwa sababu haipotezi muda wa mteja na inaweza kufanyika popote kwa simu, kompyuta kutoa fedha, kuingiza fedha kwenye akaunti, kulipia huduma, kumtumia mtu fedha na kuangalia kiasi cha fedha n.k.

ABA Banking Journal  imeeleza kuwa asilimia 42 ya miamala ya fedha inafanyika kwa njia ya mtandao huku asilimia 30 ya watu wanaofanya miamala hiyo hutumia simu kuliko kompyuta, na kwa upande wa mashine za ATM ni asilimia 5 tu ya watu ndio hutumia mashine hizo kufanya miamala.

Faida

Ikiwa mteja ana uhitaji wa kufanya muamala na hana uwezo wa kwenda benki moja kwa moja basi inakuwa rahisi kukamilisha miamala kwa kupitia mtandao ndani ya dakika chache na kuendelea na shughuli zake.

Ikiwa unatumia huduma za kibenki mtandaoni, ni rahisi kupata taarifa ya kiasi ulichonacho katika akaunti yako badala ya kwenda moja kwa moja katika benki husika.

Matumizi ya huduma za kibenki kwa njia ya mtandao humsaidia mteja kutotembea na fedha taslimu jambo ambalo muda mwingine linaweza kuwa la hatari kwa sababu si kila sehemu ni salama kutembea na fedha mkononi. Hivyo kupitia mtandao, mteja anakuwa na usalama wa fedha zake na pia anakuwa na uhakika wa kufanya malipo au miamala mingine bila kuhofia kuibiwa fedha au kuzipoteza.

Hasara

Sio kila miamala inaweza kufanyika kwa simu au kompyuta. Kwa mfano masuala ya mkopo benki humtaka mteja kufika katika tawi husika ili kuhakikisha ametoa taarifa zake zote ili kuepuka changamoto zozote zinazoweza kujitokeza.

Mitandao ni teknolojia hivyo kuna muda mteja anaweza kuwa ana shida na fedha lakini mtandao unaweza kuwa chini, au haufanyi kazi kabisa hilo likitokea basi hilo likitokea shughuli za mteja hukwama, jambo ambalo halileti picha nzuri kwa benki husika. Ni vyema ukiwa na kadi ili kama ukishindwa kufanya miamala kwenye mtandao basi utumie njia mbadala kwa mfano kutoa fedha kwenye mashine ya ATM.

Sehemu mbalimbali, ukijuana na watu ni rahisi kuekeleza mambo. Hivyo hata kwenye benki kama wafanyakazi wa benki unayotumia hawakujua basi inaweza kuwa ngumu kutatua matatizo hasa kama wewe ni mtumiaji wa huduma za kimtandao zaidi. Hivyo hata kama unatumia zaidi mtandao, tafuta namna ya kufahamiana na watu wa benki husika ili siku ukipata changamoto mtandaoni iwe rahisi kuwasiliana na watu wa benki hiyo na kutafuta suluhisho la tatizo lako.

Kutoa fedha kwa kutumia mtandao kuna kikomo chake, hivyo ikiwa mteja anataka kutoa kiasi kikubwa zaidi ya kile kilichowekwa basi atalazimika kufika katika tawi la benki ili kukamilisha muamala.

Kwa kifupi, huduma za kibenki mtandaoni zimewekwa kwa ajili ya kurahisisha maisha ya wateja, na ndio maana kuna baadhi ya benki hazikati makato pale mteja akitoa au kuweka fedha jambo ambalo linaweza kuwavutia wateja wengi. Hivyo basi, sio vibaya kutumia huduma za benki kupitia mtandao na pia kufika katika benki husika kwa ajili ya kujua mambo yanayoendelea ikiwa ni pamoja na kujipatia elimu kuhusu huduma mpya na vilevile kujifunza njia rahisi za kusuluhisha matatizo madogo.

 

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter