Ni muhimu kuwa makini kuhusu fedha hasa sehemu ya kuzihifadhia. Benki ni moja ya maeneo salama ambayo watu wengi huhifadhi fedha zao. Kuna akaunti mbalimbali ambazo mtu anaweza kuhifadhi fedha zake. Hivyo vifuatavyo ni vidokezo ambavyo vitakusaidia kuchagua akaunti bora ya akiba:
- Jiwekee malengo kuhusu akiba, kuwa na lengo na fedha unazotaka kuweka akiba kutakusaidia kufanya maamuzi kuhusu akaunti ambayo inakufaa. Ikiwa una malengo zaidi ya moja unaweza kutumia akaunti tofauti kwa kila lengo. Jambo la muhimu ni kujua sababu inayokupelekea kuweka akiba hiyo, kiasi unachotakiwa kuweka, na ni lini utahitaji fedha hizo.
- Unatakiwa kujijua mwenyewe kipindi unapolinganisha viwango (rates), kwa sababu kuna akaunti ambazo huwa zinatoa bonasi kubwa ili kukuhamasha ufungue katika akaunti hiyo, kuwa makini ni vyema ukifungua kwenye akaunti ambazo hazina mazoea/historia ya kutoa bonasi za viwango kila mara kwa sababu bonasi hizo mara nyingi huwa ni za muda mfupi. Hivyo jitahidi kufanya utafiti wa kutosha kabla hujafanya maamuzi.
- Unaweza kutumia akaunti za akiba za muda au amana za muda mrefu, hakikisha unajua lini utahitaji fedha hizo. Na ikiwa utatumia akaunti muda mrefu unatakiwa kujua kuwa riba itaongezeka na huwezi kutoa fedha zako muda wowote unaotaka (hadi mwisho wa muda uliopangwa).
- Kama hulipi kodi unashauriwa kuomba riba ya akaunti yako kulipwa ili hata kodi ikikatwa isiathiri akaunti yako. Hakikisha unapata riba nzuri kwenye kiwango ili kuepuka changamoto zozote katika masuala ya fidia za kodi.
- Kwa usalama wa fedha zako hasa zikiwa nyingi sana unashauriwa kuwekeza katika akaunti tofauti hata kwenye benki nyingine. Si lazima fedha zote uweke mahali pamoja.
Lengo la kufungua akaunti ya akiba ni kuhakikisha malengo yako yanatimia kwa mfano kuhakikisha unanunua gari, nyumba, unawasomesha watoto, n.k.